Skip to main content

RC HOMERA ATAKA TAHADHARI ZAIDI DHIDI YA CORONA


Na Mwandishi wetu.
      Katavi

KATIKA juhudi zinazofanywa na serikali ya Mkoa wa Katavi za kuendelea kukabiliana na Virus vya Corona (COVID-19) imeadaa mpango wa dharura wa kukabiliana na ugonjwa huo ambao unahitaji jumla ya fedha Tsh 856 milioni.

Akizungumza katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda Mkoani humo kwenye  kikao cha dharura PHC cha maelekezo ya namna ya kukabiliana na ugonjwa wa Corona na kusambaza muongozo wa kataratini kwa wageni,Mkuu wa Mkoa huo Comrade Juma Homera amesema janga la ugonjwa huo linapaswa kushughurukiwa ipasavyo.

Ameweka wazi kuwa suala la mpango wa dharura ni muhimu katika kuendesha mapambano dhidi ya virus vya Corona huku akisema kuwa mpango huo tayari umeshatumwa Wizara ya Afya pamoja na OR-TAMISEMI.

Amebainisha kuwa kila halmashauri za mkoa wa Katavi imeelekezwa kutenga kituo kimoja kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa sambamba na hilo kila kituo cha kutolea huduma kimeelekezwa kutenga chumba maalum ya kuwaweka wahisiwa wakati taratibu nyingine za kitabibu zikichukuliwa.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Homera (Wa pili kutoka kushoto kwenye picha) akiwa kwenye kikao cha dharura PHC cha maelekezo ya kukaniliana na ugonjwa wa corona pamoja na kusambaza muongozo wa kataratini.

Homera amewataka pia wataalamu wa afya wanapaswa kuzingatia na kufuata muongozo wa kutoa huduma za matibabu na kinga dhidi ya maabukizi ya virusi hivyo hatari kwa sababu tayari wanafahamu.

Vile vile kuimarisha mawasiliano kwa ngazi zote hususani panapotokea mhisiwa wa maabukizi ya ugonjwa wa Corona ,utaratibu wa mawasiliano unaoanzia ngazi ya familia hadi kwenye vituo cha huduma za afya.

Aidha Mkuu wa Mkoa huyo amesema kuwa maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kuhudumia wahanga wa ugonjwa huo pindi watakapoonekana kwa Mpanda Manispaa ni Rungwa Sekondari,Shule ya Sekondari ya Mpanda pamoja na  Lyamba Lyamfipa.

Wilaya ya Tanganyika ni Shule ya Sekondari Kabungu pamoja na Beach wa Kalinga Hotel ikiwa maeneo mengini ni Chuo cha Msaginya kwa Halmashauri ya Nsimbo,Usevya Sekondari kwa Halmashauri ya mMpimbwe pamoja na  Inyonga Sekondari kwa Wilaya ya Mlele.

Katika maeneo ambayo yanapakana na nchi ya DRC Congo na mikoa jirani,Idara ya uhamiaji inapaswa kuhakikisha wageni wote wanaoingia wanatambulika na kufanyiwa uchuguzi wa afya zao zifanyike na itakapo bainika wako salama taratibu za kuwarudisha kwao zifanyike.


Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Abdalah Malela amesema kuwa suala la virusi vya Corona ni vita ambayo kama mkoa inapaswa kupigana kwa kuwa na rasilimali kama vile vitendea kazi ili pasitokee kukimbiwa na Madaktari hosptalini .

Hivyo ili kupatikana kwa vitendea kazi inapaswa wadau wa afya watambue na waone umuhimu wa kuchagia fedha zitakazo fanikisha kununuliwa kwa vifaa mbalimbali vya kuwahudumia wagonjwa.

Mratibu wa huduma za tiba Mkoa wa Katavi Dkt Alex Mrema ametoa wito kwa taasisi za serikali na binafsi kutumia mifumo ya kitehama katika kufanya mikutano yao ya kikazi ambapo kwa kufanya hivyo kutaweza kuchangia kukabiliana na ugonjwa huo.

Aidha Alex amefafanua kuwa watu wana kila sababu ya kutumia mfumo wa kieletronic wa kununua na kuuza biadhaa ili kudhibiti maabukizi ya virus hivyo.

Comments

  1. Mkuu wa mkoa wa katavi Ana tujali sana mungu azidi kumpa AFYA njema sana

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

Mkuu wa Mkoa wa Katavi akibidhiwa Ofisi,aelezwa Miradi ya kusimamia.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi,Mwanamvua Hoza Mrindoko wa kwanza Kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera wakati wa makabidhiano ya Ofisi. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi Beda Katani. Wakuu wa Wilaya,Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Rachel Kasanda. Na Mwandishi Wetu,Site Tv Mapema leo Mei 25,2021 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko,amekabidhiwa Ofisi na aliye kuwa Mkuu wa Mkoa huo Juma Zuberi Homera aliye hamishiwa Mkoani Mbeya kuwa Mkuu wa Mkoa. Katika makabidhiano hayo,Homera amemtajia Mkuu wa Mkoa wa Katavi miradi ambayo inatakiwa kusimamiwa hadi ikamilike ni pamoja na Bandari ya Karema,Hosipitali ya Rufaa Mkoa,Kiwanda cha Nguo,Jengo la Utawala pamoja na Umeme wa Gridi ya Taifa. Aidha,amesema Katavi ni Nyumbani hivyo atatoa ushirikiano kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi huku akiwakaribisha Viongozi na Wananchi kwa ujumla katika Mkoa wa Mbeya. "Kuna hili la Gridi ya Taifa ambalo linaendelea,kuna Kiwan...

Tabasamu hili kwa Wanafunzi,Nuru imewaka Juu yao/Mwekezaji afanya Jambo ...

Ajira Mpya Wakaribishwa Mlele, Full Kula Bata/Makubwa yaja