Ni baada ya wahamiaji haramu watano waliokamatwa na maafisa wa uhamiaji kushindwa kufanyiwa vipimo.
Na Mwandishi Wetu,
Katavi.
MGANGA Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Omary Sukari anapaswa kujieleze kutokana na kukiuka maagizo aliyopewa March 28 mwaka huu kwenye kikao cha dharura PHC cha maelekezo ya kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na virusi vya Corona.,
Kikao hicho ambacho kililenga pia kusambaza muongozo wa karatini kwa wageni wote wanaoingia mkoani humo kupitia njia mbali mbali za usafiri kama vile wa mabasi na meli ambapo yalitolewa maadhimio ya kuhakikisha kila eneo la mpaka wa Mkoa linakuwa na kituo maalumu cha kizuizi kwa ajili ya ukaguzi wa kitabibu na karatini pamoja na wataalamu wa afya ili kabla ya mtu hajaingia mjini apimwe kwanza.
Akitoa kauli hiyo Mkuu wa Mkoa wa Katavi Comrade Juma Homera baada ya kufanya
ukaguzi wa kushitukiza ili kuona utekelezaji wa maagizo yake katika kituo cha kizuizi cha Milala ambapo hakukuta muuguzi yeyote wa afya mahali pale
Licha ya kutoa maagizo hayo kwa maafisa hao kujieleza haraka iwezekanavyo ameitaka idara ya afya ihakikishe inaweka vizuizi huku wakiwepo na wauguzi ambao watakuwa na kazi maalumu ya kupima watu wote wanaoingia mkoani humo na wale watakao bainika kuwa na vurusi vya corona wawezi kuwekwa kwenye karatini.
Vilevile amevitaka vyombo vya usalama mkoani Katavi kuhakikisha vinafanya ukaguzi wa kutosha ili kutambua raia wanaoingia wanatambulika.
Katika idara ambayo imefanikiwa kutekeleza maagizo ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Homera ni Idara ya uhamiaji pekee.
![]() |
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Homera |
Kamishina Msaidizi wa uhamiaji Mkoa wa Katavi Vicent Haule amesema baada ya kupata maagizo
hayo ya Mkuu wa Mkoa mara moja walitekeleza maagizo kwa sababu wanatambua umuhimu wa suala hilo ili kuweza kukabiliana na kuenea kwa kwa virusi vya corona
Vicent amebainisha kuwa wamefanikiwa kukamata wahamiaji haramu watano ambao walitaka kuvuka kinyume cha utaratubu wa sheria za nchi huku juhudi za kupimwa ziligonga mwamba kwa kuwa kwenye kituo hicho cha Milala hapakuwa na muuguzi hata mmoja wa afya.
![]() |
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Omary Sukari |
Nao baadhi ya wananchi kwa wakati tofauti Paulina Mwasha,Anthony na Wande Juma wamesema kuwa kitendo cha kukosekana kwa wahudumu wa afya katika vizuizi ni hatari sana kwa mkoa wa Katavi kwani kunauwezekano watu wenye maabukizi ya virusi vya corona wakaingia.
Hivyo wamemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Homera kwa kuchukua hatua sitahiki za kumtaka mganga mkuu wa Mkoa kutoa maelezo ya kutosha kuwa kwanini ameruhusu uzembe kama huo ujitokeze huku akifahamu kuwa dunia iko kwenye mapambano dhidi ya corona.
Comments
Post a Comment