Baadhi ya Wadau wakisikiliza jambo kwa makini katika Kikao Kazi cha Wadau wa Afya kilichofanyika Mei 20,2021 katika Ukumbi wa Mpanda Manispaa. Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Katavi Bi. Crecensia Joseph akiwahutubia Wadau wa Afya,katika Kikao Kazi cha Wadau wa Afya. Na Mwandishi Wetu,Site Tv Mpanda-Katavi. Mkoa wa Katavi umeweka Mkakati wa Miaka Mitano wa kupunguza Vifo vya Mama na Mtoto ambapo jumla ya Watoto Wachanga 631 walifariki Dunia kwa kipindi cha Januari hadi Desemba 2020 na 93 walifariki kipindi cha Januari hadi Machi 2021. Akitoa hotuba Jana Mei 20,2021 mbele ya Wadau mbalimbali wa Afya Mkoani Katavi katika kikao Kazi cha Wadau wa Afya,Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Katavi Crecensia Joseph amesema Vifo 56 vilivyotokana na Uzazi vilisababishwa na kutokwa na Damu nyingi kabla na baada ya kujifungua Vifo 22,Kifafa cha Mimba Vifo 6 na Upungufu mkubwa wa Damu wakati wa Ujauzito Vifo 5. Aidha,amezitaja sababu zingine kuwa ni uambukizo mkali baada ya kujifungua Vifo 10 na Magonjwa mengine...
Karibu kwenye Blog Yetu na tupo tayari kukuhabarisha kwa Habari na Matukio mbalimbali kwa Weledi Masaa 24 popote ulipo,kama una taarifa au unataka kutangaza na Sisi tafadhali wasiliana nasi kupitia ukurasa huu. Pia tunapatikana YouTube @sitetvtz,Instagram,Twitter na Facebook @sitetvtz. Ofisi zetu zipo Jengo la Mpanda Plaza Ghorofa ya 3,Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi.