Na Zainabu Mtima,Site Tv-Mlele
Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi wamekutana kujadili shughuli za maendeleo katika robo Tatu ya Mwaka wa Fedha 2021.
Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa ni
pamoja na utekelezaji wa miradi mbalimbali katika Kata zote Sita za Halmashauri
hiyo.
Akizungumza katika Baraza hilo Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Mlele Soud Mbogo amesema kumekuwa na changamoto ya uchache wa
Wataalamu wa ukaguzi wa Nyama jambo lililomfanya atoe azimio la kuwatoa kwenye
huduma ya ukaguzi wa nyama wataalamu wote waliopo sasa na kutafutwa wengine
watakaofanya kazi kwa uweledi.
Akitolea ufafanuzi changamoto hiyo Afisa
Mifugo na Uvuzi wa Wilaya,Livingstone Mandari amesema Idara ya Mifugo na Uvuvi inaupungufu mkubwa wa Watumishi
jambo linalowafanya waelemewe na kazi ya ukaguzi wa Nyama.
Aidha Livingstone ameongeza kuwa ukaguzi
wa Nyama unatakiwa ufanywe na mtaalam aliyesomea Afya ya Wanyama ambapo kwa Halmshauri
nzima ya Wilaya ya Mlele yuko Mtaalamu Mmoja tu .
Hata hivyo Afisa Mifugo amesema
changamoto ilipotokea kwa wachinjaji ni kutofahamu uchache wa wakaguzi wa Nyama
uliopo kwani waliopo hufanya kazi zaidi ya Moja.
Hapo uvumilivu unaitajika kupata watalam wengine
ReplyDelete