Skip to main content

WAKAGUZI WA NYAMA WANATUZINGUA.

Na Zainabu Mtima,Site Tv-Mlele

Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi wamekutana kujadili shughuli za maendeleo katika robo Tatu ya Mwaka wa Fedha 2021.

Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa ni pamoja na utekelezaji wa miradi mbalimbali katika Kata zote Sita za Halmashauri hiyo.

Akizungumza katika Baraza hilo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mlele Soud Mbogo amesema kumekuwa na changamoto ya uchache wa Wataalamu wa ukaguzi wa Nyama jambo lililomfanya atoe azimio la kuwatoa kwenye huduma ya ukaguzi wa nyama wataalamu wote waliopo sasa na kutafutwa wengine watakaofanya kazi kwa uweledi.

Akitolea ufafanuzi changamoto hiyo Afisa Mifugo na Uvuzi wa Wilaya,Livingstone Mandari amesema Idara ya Mifugo  na Uvuvi inaupungufu mkubwa wa Watumishi jambo linalowafanya waelemewe na kazi ya ukaguzi wa Nyama.

Aidha Livingstone ameongeza kuwa ukaguzi wa Nyama unatakiwa ufanywe na mtaalam aliyesomea Afya ya Wanyama ambapo kwa Halmshauri nzima ya Wilaya ya Mlele yuko Mtaalamu Mmoja tu .

Hata hivyo Afisa Mifugo amesema changamoto ilipotokea kwa wachinjaji ni kutofahamu uchache wa wakaguzi wa Nyama uliopo kwani waliopo hufanya kazi zaidi ya Moja.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

Tabasamu hili kwa Wanafunzi,Nuru imewaka Juu yao/Mwekezaji afanya Jambo ...

Ajira Mpya Wakaribishwa Mlele, Full Kula Bata/Makubwa yaja

Katavi Yakemea Vikali Ushoga,Mauaji "Wanaume Msiwazuie Wake Zenu Kufanya...