Skip to main content

RAIS DK.MWINYI AMEFANYA ZIARA MAENEO YA MRADI WA MANGAPWANI.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amefanya ziara katika eneo linalotarajiwa kujengwa bandari mpya ya Magapwani na kueleza kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itatoa maamuzi yenye tija kwa ajili ya muendelezo wa eneo hilo.

Rais Dk. Mwinyi aliyasema hayo jana Mei 18,2021, mara baada ya kufanya ziara ya kulitembelea eneo linalotarajiwa kujengwa bandari mpya ya Mangapwani, Wizaya ya Kaskazini B,Mkoa wa Kaskazini Unguja ambapo pia, alitembelea miradi ambayo imeanza kabla ya ujenzi huo mpya.

Katika maelezo yake Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa Serikali itakuja na maamuzi yenye tija ambayo yatasaidia kwa pande sote mbili ikiwemo upande wa wawekezaji ambao walianza kuekeza kwa muda mrefu katika eneo hilo pamoja na kwa upande wa Serikali kwa ujumla huku akiwataka wawekezaji hao kuwa na subira .

Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa Serikali imeridhishwa na ukubwa wa eneo pamoja na hatua ya awali iliyofikiwa na kuelez ajambo kubwa lililompelekea kufanya ziara hiyo hivi leo ikiwa ni kwenda kujiridhisha na kulielewa vyema eneo hilo.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi aliwasisitiza wawekezaji hao kuwa na subira huku akisema kwamba atahakikisha jambo hilo linakwenda kwa haraka na ameahidi kukaa na wahusika mapema iwezekanavyo kwa azma hiyo hiyo ya kuharakisha mradi huo.

Alitumia fusra hiyo kutoa shukurani kwa wananchi wa eneo hilo kwa utayari wao waliouonesha kwa kuruhusu maendeleo kwa kushirikiana na Serikali yao kwa kuupisha mradi huo mkubwa wa bandari.

Pia, Rais Dk. Mwinyi alitoa shukurani kwa wataalamu pamoja na washauri elekezi kwa kumaliza hatua ya mwanzo kwa kipindi cha miezi mitatu huku akieleza hatua zitakazofuata hivi sasa sambamba na maamuzi yatakayochukuliwa.

Aliongeza kwamba Serikali inafanya juhudi hizo kwa kuamini kwamba hivi sasa Bandari ya Malindi haikidhi haja tena na ndio maana imeamua kuanzisha mradi huo mkubwa wa Bandari ya Mangapwani kwa maendeleo ya Zanzibar.

Katika ziara yake hiyo, Rais Dk. Mwinyi alitembelea eneo la mradi wa Chelezo, Mradi wa Islana Petroleum, Mradi wa Salama International Company na eneo la Mradi wa TP Invetment Depot na kupata maelezo kutoka kwa viongozi wa Serikali na wawekezaji.

Akiwa katika eneo hilo, Mapema alipata maelezo ya mradi huo kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Amour Hamil Bakari ambaye alimueleza namna ya michoro ya mradi huo zinavyoelekeza huku Katibu Tawala wa Mkoa huo wa Kaskazini Unguja Makame Machano Haji akieleza namnawalivyoshirikiana na mshauri elekezi kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Nao wawekezaji wa eneo hilo ambao walianza kuekeza miradi yao kabla ya kuanzishwa kwa mradi huo mkubwa kwa nyakati tofauti walimueleza Rais Dk. Mwinyi hatua walizofikia katika miradi yao huku wakionesha utayari wao wa kuendelea kushirikiana na Serikali.

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Ayoub Mohammed Mahmoud alitumia fursa hiyo kumkaribisha Rais Dk. Mwinyi katika Mkoa huo pamoja na kueleza hatua zilizofikiwa na mradi huo kwa mashirikiano na wataalamu wa Wizara husika wakiongozwa na Waziri wa Wizara hiyo Rahma Kassim Ali.

Mnamo Mei 07, 2021 Rais Dk. Mwinyi alipokea Mpango wa ujenzi wa Bandari ya kisasa ya Mangapwani kutoka Mamlaka ya Uwekezaji ya Oman (OIA), chini ya Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo Sheikh Mohammed Al Tooq ambapo mradi huo unahusisha maeneo makuu matatu, ikiwemo ujenzi wa Bandari mbali mbali, mji wa kisasa wa makaazi pamoja na Mpango wa kuiendeleza Bandari ya Malindi ili iweze kutumika kama Bandari ya utalii.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822

E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

Comments

Popular posts from this blog

WAJASIRIAMALI MPANDA WAILILIA SERIKALI KUCHELEWA UPATIKANAJI WA VITAMBULISHO

Na Swaumu Katambo, Katavi W afanyabiashara wadogo   katika stendi ya mabasi M izengo P inda wameiomba S erikali kuharakisha ugawaji wa vitambulisho ili kuep u kana na adha ya kulipa ushuru wa H almashauri ambao una   gharama  kubwa. W akizungumza na Site Tv  wajasiriamali M jini M panda wame i lalamikia H almashauri ya M anispaa ya M panda kuwatoza ushuru pasipo kuwa na utaratibu wowote . Mkurugenzi wa M anispaa ya M panda M ichael N zyungu amesema kuwa adha hiyo imetokana na kuchele we shwa kwa vitambulisho na amewataka wajasiriamali kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki. Vitambulisho vya ujasiriamali vilianzishwa na serikali maalumu kwa kuwasaidia wafanya   biashara wadogo kutoa huduma bila bugdha yoyote . MWISHO

Tufanye mabadiliko ya kina kwenye mfumo wa elimu -Mbunge Rose Tweve

KANISA KATOLIKI PAROKIA YA INYONGA LAFANYA MISA MAALUMU KUMUOMBEA DKT MAGUFULI, DC JAMILA ASISITIZA KUMUENZI KWA VITENDO

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda  ambaye pia ni  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mlele  Mhe  Jamila Yusu ph akisisitiza jambo wakati  akizungumza kwenye Misa Maalumu katika Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Mkuu wa Wilaya ya Mpanda  ambaye pia ni  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mlele  Mhe  Jamila Yusu ph akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Kanisa katoliki Parokia ya inyonga mara baada ya kumalizika  Misa Maalumu ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Kiongozi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga Padri  Maricelo Butoyi akiongoza Misa Maalumu ya  kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Sehemu ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga wakifuatilia ibada Maalumu ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Sehemu ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga wakifuatilia ibada Maalumu ...