Baadhi ya Wadau wakisikiliza jambo kwa makini katika Kikao Kazi cha Wadau wa Afya kilichofanyika Mei 20,2021 katika Ukumbi wa Mpanda Manispaa.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Katavi Bi. Crecensia Joseph akiwahutubia Wadau wa Afya,katika Kikao Kazi cha Wadau wa Afya.
Na Mwandishi Wetu,Site Tv Mpanda-Katavi.
Mkoa wa Katavi umeweka Mkakati wa Miaka Mitano wa kupunguza Vifo vya Mama na Mtoto ambapo jumla ya Watoto Wachanga 631 walifariki Dunia kwa kipindi cha Januari hadi Desemba 2020 na 93 walifariki kipindi cha Januari hadi Machi 2021.
Akitoa hotuba Jana Mei 20,2021 mbele ya Wadau mbalimbali wa Afya Mkoani Katavi katika kikao Kazi cha Wadau wa Afya,Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Katavi Crecensia Joseph amesema Vifo 56 vilivyotokana na Uzazi vilisababishwa na kutokwa na Damu nyingi kabla na baada ya kujifungua Vifo 22,Kifafa cha Mimba Vifo 6 na Upungufu mkubwa wa Damu wakati wa Ujauzito Vifo 5.
Aidha,amezitaja sababu zingine kuwa ni uambukizo mkali baada ya kujifungua Vifo 10 na Magonjwa mengine kama matatizo ya Moyo wakati wa Ujauzito, Malaria n.k Vifo 13.
Bi.Crecensia pia amezitaja changamoto kadhaa zinazochangia Vifo hivyo ni kutokuwa na Vipimo muhimu kwa Mama Wajawazito wanapo hudhuria Kliniki,kutokuwa na usafiri wa dharura kwa baadhi ya Vituo vya kutolea huduma,Wajawazito kuchelewa kujiandikisha katika Vituo vya kutolea huduma za Afya na uelewa mdogo kwa akina Mama na Jamiii kwa ujumla juu ya umuhimu kujifungulia katika Vituo vya kutolea huduma za Afya.
Hata hivyo,amesema Jumla ya Vifo 56 vitokanavyo na Uzazi vimetokea katika Mkoa wa Katavi kwa muda wa kipindi cha Januari hadi Disemba 2020 na Vifo 11 kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2021.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt.Omary Sukari amesema kupoteza akina Mama 54 ni sawa na Basi Moja lililopinduka na kuwapoteza wakina Mama jambo ambalo linasikitisha hivyo lipo jukumu la kuunganisha nguvu na Wadau mbalimbali ili kutokomeza Vifo hivyo.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Omary Sukari,akifafanua jambo.
Comments
Post a Comment