Skip to main content

Aliyekodi watu na kumuua baba yake ahukumiwa kunyongwa.

kunyongwa pcMahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, imemhukumu Seni Lisesi adhabu ya kunyongwa hadi kufa baada ya kumtia hatiani kuhusika na mauaji ya baba yake mzazi.

Lisesi (33) mkazi wa Kijiji cha Mwadui wilayani Sumbawanga, alidaiwa kuhusika kwenye mauaji ya baba yake Lisesi Magadula (50) ili arithi mali.

Hukumu hiyo imetolewa jana Jumanne ya Mei 18, 2021 na Jaji wa Mahakama hiyo Dustan Ndunguru baada ya kuridhika na ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashitaka ukiongozwa na mawakili wa Serikali, Njoloyota Mwashubila na Irene Mwabeza.
Kwa mujibu wa hati ya mashitaka iliyowasilishwa mahakamani hapo, inaeleza kuwa Lisesi alitenda kosa la mauaji ya Magadula kwa kushirikiana na kikundi cha watu.
Ilidaiwa kuwa Liseni alikodisha kikundi hicho kwa ajili ya kufanya mauaji hayo mnamo Desemba 4, 2016 nyumbani kwa marehemu huko Kijiji cha Mwadui.
Ilidaiwa na waendesha mashitaka wa Serikali kwamba muuaji akiwa na wenzake walivamia nyumbani kwa Liseni nyakati za usiku wakiwa silaha aina ya mapanga na kumkatakata hadi kufariki huku lengo likiwa ni kurithi mali mbalimbali ikiwemo ng'ombe na mashamba.
Hata hivyo, Polisi katika uchunguzi wao walimtia mbaroni Liseni na kumfikisha katika vyombo vya sheria.
Katika kesi hiyo, upande wa mashitaka ulipeleka mashahidi wanne huku Lisesi akiwakilishwa na Wakili wa kujitegemea Neema Charles, ambapo alijitetea kuwa hakushiriki katika mauaji hayo akiiomba mahakama kumuachia huru.
Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, waendesha mashitaka wa Serikali waliomba mahakama kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia za kushiriki kukatisha uhai wa wazazi wao kwa tamaa za kurithi mali.
Akisoma hukumu hiyo, Jaji Ndunguru alisema ameridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo pasi kuacha shaka na amemkuta mtuhumiwa na hatia ya kufanya mauaji ya kukusudia hivyo kwa kutumia kifungu cha 196 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 na kifungu cha 197 anahukumiwa kunyongwa hadi kufa.
CHANZO:GAZETI LA MWANANCHI

Comments

Popular posts from this blog

Mkuu wa Mkoa wa Katavi akibidhiwa Ofisi,aelezwa Miradi ya kusimamia.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi,Mwanamvua Hoza Mrindoko wa kwanza Kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera wakati wa makabidhiano ya Ofisi. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi Beda Katani. Wakuu wa Wilaya,Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Rachel Kasanda. Na Mwandishi Wetu,Site Tv Mapema leo Mei 25,2021 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko,amekabidhiwa Ofisi na aliye kuwa Mkuu wa Mkoa huo Juma Zuberi Homera aliye hamishiwa Mkoani Mbeya kuwa Mkuu wa Mkoa. Katika makabidhiano hayo,Homera amemtajia Mkuu wa Mkoa wa Katavi miradi ambayo inatakiwa kusimamiwa hadi ikamilike ni pamoja na Bandari ya Karema,Hosipitali ya Rufaa Mkoa,Kiwanda cha Nguo,Jengo la Utawala pamoja na Umeme wa Gridi ya Taifa. Aidha,amesema Katavi ni Nyumbani hivyo atatoa ushirikiano kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi huku akiwakaribisha Viongozi na Wananchi kwa ujumla katika Mkoa wa Mbeya. "Kuna hili la Gridi ya Taifa ambalo linaendelea,kuna Kiwan...

Tabasamu hili kwa Wanafunzi,Nuru imewaka Juu yao/Mwekezaji afanya Jambo ...

Ajira Mpya Wakaribishwa Mlele, Full Kula Bata/Makubwa yaja