Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mbwana Saleh Mhando akizungumza na waadishi wa habari ofisini kwake huku akihimiza wananchi kujikinga na ugonjwa wa COVID 19 pamoja na EBOLA. Na George Mwigulu,Tanganyika. Wananchi wa Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi wametakiwa kuendelea kuchukua hatua madhubuti za kupambana na kujikinga na ugonjwa wa COVID 19 pamoja na Ebola wawapo sehemu za mikusanyiko hususani minadani. Hayo aliyasema Mkuu wa wilaya ya hiyo Mbwana Saleh Mhando wakati akizungumza na Wanahabari ofisi kwake katika kata ya Ifukutwa ambapo aliwataka wakazi hao kuwa waangalifu pamoja na kuchukua tahadhari kubwa wakati huu ugonjwa wa corona unapoendelea kuenea hapa nchini. Mkuu wa wilaya hiyo alieleza kuwa kutokana na wilaya ya Tanganyika kupakana na nchi ya DRC Congo ambayo imeshuhudiwa pia na maambukizi ya COVID 19 pamoja na ugonjwa wa Ebola.Hatua madhubuti zinatakiwa kuchukuliwa na wananchi za kujikinga pasipo kuiachia jukumu hilo pekee serikal...
Karibu kwenye Blog Yetu na tupo tayari kukuhabarisha kwa Habari na Matukio mbalimbali kwa Weledi Masaa 24 popote ulipo,kama una taarifa au unataka kutangaza na Sisi tafadhali wasiliana nasi kupitia ukurasa huu. Pia tunapatikana YouTube @sitetvtz,Instagram,Twitter na Facebook @sitetvtz. Ofisi zetu zipo Jengo la Mpanda Plaza Ghorofa ya 3,Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi.