Skip to main content

WAHUKUMIWA JELA KIFUNGO CHA MAISHA KWA KOSA LA UBAKAJI













Na Mwandishi Wetu







Katavi
 Mahakama ya Hakimu  Mkazi Katavi imewahukumu watu wawili  Swalehe Idd(29( Mkazi wa Mtaa wa Ilembo na  Mess Ntinka (23)mkazi wa Mtaa wa Kasimba tumikia kfungo cha maisha  jela baada ya kupatikana na hatia  ya kumbaka kwa kushirikiana zamu zamu msiichana mwenye   umri wa miaka 15 kwenye stendi ya mabasi ya Manispaa ya Mpanda ya Mizengo Pinda   

  Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu MkazI mfawidhii wa Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Katavi Emanuel  Ngigwana baada ya Mahakama kuridhika na ushahidi uliotplewa mahakamani hapo na upande wa  mashitaka ulikuwa ukiongozwa na mwendesha mashitaka wa kutoka ofisi ya  mwendesha mashitaka Mkoa wa Katavi   Lungano Mwasubila

 Washitakiwa hao wote wawili wamehukumu kutumikia kifungo hicho cha maisha jela kuanzia jana baada ya kupatikana na hatia ya kutenda kosa la kifungu cha sheria namba 131 (1) (131A)   (2) sura ya 16 cha shereria ya majejeo ya mwaka 2002

  Awali kwenye kesi hiyo mwendesha mashitaka huyo alidai kuwa washitakiwa hao walitenda kosa hilo hapo  januari  24 mwaka huu   majira ya saa   huko katika eneo la stendi kuu ya mabasi ya Mkoa wa Katavi Mizengo Pinda iliyoko katika Mtaa wa Ilembo Manispaa ya Mpanda

 Siku hiyo ya tukio msichana huyo alikuwa akitokea Mkoani Songwe kama abiria akiwa anaelekea Mkoani Kigoma chini ya uangalizi wa Kondakta wa basi hilo alilokuwa akisafiria .

 Mwendesha mashita MwasubIla alieleza kuwa baada ya msichana huyo kuwa amefika kwenye stendi ya Mizengo Pinda walijitokeza washitakiwa hao ambao walikuwa ni  maajenti wa mabasi yaendayo Mikoani na kumweleza  kondakta huyo kuwa wao ni maafisa wa usalama wa stendi hiyo hivyo wanamwomba binti huyo awe mikononi mwao kwani atakuwa yuko kwenye mikono salama hadi hapo siku ilifuata ambayo wangemsafirisha kwenda kwao kigoma kwa mabasi yaendayo huko .

  Baada ya kuwa wamekabidhi  binti huyo washitakiwa hao walimchukua na kumpeleka hadi kwenye chumba kimoja kilichopo kwenye stendi hiyo na kisha walianza kumbaka kwa zamu zamu hadi hapo walipomaliza  haja yao .

 Mwendesha mashitaka alidai kuwa baada ya kuwa wamemfanyia kitendo hicho walimtolea  maneno ya vitisho kuwa asiwaambie watu vinginevyo watamuuwa hata hivyo baada ya kuwa amefika Mkoani Kigoma kwa wazazi wake aliwaeleza  jinsi alivyofanyiwa kitendo hicho kwa kubakwa ndipo taarifa zilitolewa polisi na watuhumiwa walianza kusakwa na kukamatwa.

 Upande wa mashitaka kwenye kesi hiyo ulikuwa na mashahidi wanne akiwemo daktari  aliyemfanyia uchunguzi msichana huyo pamoja na muhanga mwenyewe wa tukio hilo.

 Kabla ya kutowa hukumu hiyo hakimu Mkazi  Mfawidhi wa Mahakama ya  Hakimu Mkazi  Katavi  Emanuel Ngigwana alitowa nafasi kwa watuhumiwa kuweza kujitetea kama wanayosababu ya msingi ya kuwafanya wapunguziwe adhabu .

 Katika utetezi wao waliiomba mahakama iwapunguzie adhabu kwa kile walchodai kuwa  wanafamilia ambayoinawategemea na pia umri wao ni mdogo  maombi hayo ambayo yalipingw na mwendesha mashitaka Mwasubila ambae aliiomba mahakama itowe adhabu kali kwa washitakiwa 

 Hakimu  Ngiwana baada ya kusikiliza utetezi huo aliiambia Mahakama kuwa kosa walilopatikanalo watumiwa kifungo chake ni cha kutumikia kwenda jela maisha


Comments

Popular posts from this blog

WAJASIRIAMALI MPANDA WAILILIA SERIKALI KUCHELEWA UPATIKANAJI WA VITAMBULISHO

Na Swaumu Katambo, Katavi W afanyabiashara wadogo   katika stendi ya mabasi M izengo P inda wameiomba S erikali kuharakisha ugawaji wa vitambulisho ili kuep u kana na adha ya kulipa ushuru wa H almashauri ambao una   gharama  kubwa. W akizungumza na Site Tv  wajasiriamali M jini M panda wame i lalamikia H almashauri ya M anispaa ya M panda kuwatoza ushuru pasipo kuwa na utaratibu wowote . Mkurugenzi wa M anispaa ya M panda M ichael N zyungu amesema kuwa adha hiyo imetokana na kuchele we shwa kwa vitambulisho na amewataka wajasiriamali kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki. Vitambulisho vya ujasiriamali vilianzishwa na serikali maalumu kwa kuwasaidia wafanya   biashara wadogo kutoa huduma bila bugdha yoyote . MWISHO

Tufanye mabadiliko ya kina kwenye mfumo wa elimu -Mbunge Rose Tweve

KANISA KATOLIKI PAROKIA YA INYONGA LAFANYA MISA MAALUMU KUMUOMBEA DKT MAGUFULI, DC JAMILA ASISITIZA KUMUENZI KWA VITENDO

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda  ambaye pia ni  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mlele  Mhe  Jamila Yusu ph akisisitiza jambo wakati  akizungumza kwenye Misa Maalumu katika Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Mkuu wa Wilaya ya Mpanda  ambaye pia ni  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mlele  Mhe  Jamila Yusu ph akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Kanisa katoliki Parokia ya inyonga mara baada ya kumalizika  Misa Maalumu ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Kiongozi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga Padri  Maricelo Butoyi akiongoza Misa Maalumu ya  kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Sehemu ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga wakifuatilia ibada Maalumu ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Sehemu ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga wakifuatilia ibada Maalumu ...