Skip to main content

DC MATINGA ATANGAZA VITUO VYA KUNUNULIA MAZAO HUKU ALIPIGA MARUFUKU KUFANYA BIASHARA BILA LESENI








Na  George Mwigulu
           Katavi .

 Serikali ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi imetangaza vituo  65 vitakavyo tumika kwa ajiri ya ununuzi wa mazao mbalimbali katika msimu huu wa kilimo wa 2019/ 2020 na vituo  16 vya mazao ya stakabadhi gharani ili kumfanya mkulima asiibiwe na kuzifanya Halmashauri za Wilaya hiyo kudhibiti mapato yake na pia imepiga marufuku mfanya biashara yeyote kununua mazao bila kuwa na leseni

 Vituo hivyo vilitangazwa hapo Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Lilian Charles Matinga wakati alipokuwa akiongea na  wandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali vilivyopo katika Mkoa huu kikao ambacho kilihudhuliwa pia na Wakurugenzi wa Halmashauri  za  Manispaa ya Mpanda na Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo


 Alisema  Halmashauri  mbili zilizopo katika Wilayah ii wamekuwa wakipoteza mapato yao  kutokana na wafanya biashara wanao nunua   mazao kwenye Halmashauri hizo  kuwa wadanganyifu na kuzifanya Halmashauri kupoteza mapato   pia  mkulima amekuwa akipunjika bei kutokana na wafanya biashara kununua mazao bila kuwa na vipimo halali vya  mizani.

 Lengo la  kuweka vituo  hivyo  ni kutataka Halmashauri ziweze kukusanya  mapato vizuri  pamoja na fedha za maendeleo na kumsaidia mkulima asipunjwe kwenye bei na vipimo ambapo apo awali wafanya biashara walikuwa wakinunua mazao kwa kutumia ndoo ambazo sio vipimo halisi
.
 Matinga alifafanua kuwa  jumla ya vituo 53 vimeandaliwa kwa ajiri ya ununuzi wa mazao ya Mahindi   , Karanga ,  Mpunga  na  muhogo katika Halmashauri hizo mbili  ambapo  Manispaa ya Mpanda itakuwa na vituo 26 na Halmashauri ya  Wilaya ya Nsimbo itakuwa na vituo 27.
 Pia wameweka vituo 16 kwa ajiri ya mazao  ya  yatakayo uzwa kwa stakabadhi gharani  kwenye Halmashauri hizo ambapo mazao hayo yatahusu   ufuta na alizeti .

DC  Matinga alisisitiza kuwa  hakuna mfanyabiashara yeyote ambae ataruhusiwa kununa mazao kwenye Wilaya hiyo bila kuwa na leseni ya biashara kutoka kwenye Halmashauri husika  pia amepiga marufuku   wafanya biashara kununua mazao kwa kutumia ndoo za plasitiki wala kutumia mizani ambayo haija  kaguliwa.

Amepiga marufuku kwenye maeneo hayo watu ambao wamekuwa wakijifanya wao kuwa ni madalali wa kuwanunulia wafanya biashara mazao kuwepo kwenye vituo hivyo kwani wamekuwa wakisababisha mkulima kuibiwa

Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Michael Nzyungu  alisema Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda imeweka utaratibu wa mtu kwa wafanya biashara anae taka kununu mazao  ni lazima awe na leseni ya biashara ya kununua mazao hayo ambayo atakuwa analipia  leseni  tshs 100,000 .

 Alifafanua kuwa   mazao  ambayo yatakuwa ni ya mkulima ambayo hayazidi tani moja  hawata yatoza ushuru kama ambavyo Rais alivyoagiza isipokuwa kwa mfanyabiashara yeyote atakae nunua atatozwa ushuru hata kama mazao hayazidi tani moja .

Aliwaonya wafanya biashara ambao watafanya ujanja wa kufanya biashara bila kuwa na leseni watambue kuwa endapo watakamatwa mazao yao yote yatataifishwa.

 Alisema kwa wale wafanya biashara watakao kuwa wamenunua mazao kwenye Halmashauri hiyo na kutaka kuyasafirisha nje ya Mkoa wa Katavi ni lazima wawe na kibali ambacho kitakuwa kinatolewa na Mkuu wa Wilaya
 

Comments

Popular posts from this blog

Mkuu wa Mkoa wa Katavi akibidhiwa Ofisi,aelezwa Miradi ya kusimamia.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi,Mwanamvua Hoza Mrindoko wa kwanza Kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera wakati wa makabidhiano ya Ofisi. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi Beda Katani. Wakuu wa Wilaya,Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Rachel Kasanda. Na Mwandishi Wetu,Site Tv Mapema leo Mei 25,2021 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko,amekabidhiwa Ofisi na aliye kuwa Mkuu wa Mkoa huo Juma Zuberi Homera aliye hamishiwa Mkoani Mbeya kuwa Mkuu wa Mkoa. Katika makabidhiano hayo,Homera amemtajia Mkuu wa Mkoa wa Katavi miradi ambayo inatakiwa kusimamiwa hadi ikamilike ni pamoja na Bandari ya Karema,Hosipitali ya Rufaa Mkoa,Kiwanda cha Nguo,Jengo la Utawala pamoja na Umeme wa Gridi ya Taifa. Aidha,amesema Katavi ni Nyumbani hivyo atatoa ushirikiano kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi huku akiwakaribisha Viongozi na Wananchi kwa ujumla katika Mkoa wa Mbeya. "Kuna hili la Gridi ya Taifa ambalo linaendelea,kuna Kiwan...

Tabasamu hili kwa Wanafunzi,Nuru imewaka Juu yao/Mwekezaji afanya Jambo ...

Ajira Mpya Wakaribishwa Mlele, Full Kula Bata/Makubwa yaja