Na Mwandishi wetu
IRINGA
MAUWAJI ya kinyama
yafanyika usiku wa ijumaa kuu
Mkoa wa Iringa eneo la Kijiweni kata ya
Kwakilosa katika Manispaa ya Iringa baada ya
mhubiri wa injili na mgombea ubunge mtarajiwa
katika jimbo la Kalenga Raymond Mdota
(46) kuuwawa kwa kuchinjwa shingo yake akiwa
katika huduma ya kuhubiri injili
kwenye klabu cha Pombe za kienyeji na mwili wake
kutupwa kwenye mahindi.
Mashuhuda wa tukio hilo waliozungumza
na mwandishi wa habari hizi eneo
la tukio walisema kuwa tukio hilo
lilitokea usiku wa Ijumaa na nje
ya chumba kimoja wapo cha klabu cha pombe
za kienyeji kijulikanacho kwa jila la Kijiweni
Klabu .
Walisema kuwa kabla ya mauwaji hayo
Mdota ambae ni mmoja kati ya walimu wastaafu
alifika katika eneo hilo la Klabu cha
Kijiweni akiwa na radio yake kubwa aliyokuwa
akiitokota huku ikiwa inapiga
nyimbo za dini na
kuanza kuzunguka chumba kimoja hadi baada
ya kingine akipiga muziki wa dini
ya kikristo kwa ajili ya kuomboleza mateso
ya Yesu Kristo na nyingine za kufufuka kwa
Yesu .
“ Yaania alifika hapa mida kama ya saa
mbili usiku akiwa na radio yake kubwa akipiga nyimbo za
dini kwa sauti kubwa huku akicheza kwa fuhara na
kuwasisitiza watu kuachana na dhambi na kumgeukia Mungu
tulimfurahia sana hasa ukizingatia ilikuwa ni
ijumaa kuu ya mateso ya Yesu ila muda ulipozidi kusogea
katika radio
hiyo hiyo alianza kupiga nyimbo za muzidi wa
kidunia na kuanza kutangaza siasa kuwa yeye ni mkazi wa Magumbike na
anampango wa kwenda kugombea ubunge wa jimbo la kalenga"
alisema mmoja kati ya mashuhuda ambae hakutaka kutaja jina lake.
Alisema wakati akihubiri injili
alikuwa ameshika rozari yake mkononi ila
baadae alipokuwa akitangaza siasa alishika
skafu yenye rangi ya bendera ya
Taifa huku akisisitiza kuwa yeye ndie
mbunge mpya wa kalenga bila kutaja
kupitia chama gani na
wakati huo akinywa pombe aina ya
Ulanzi na kuwanunulia watu pombe huku
akicheza muziki .
Hata hivyo alisema wakati muda
wa kufunga klabu hicho ukielekea kufika
wao waliondoka na kumwacha yeye
na watu wachache wakiendelea kuwepo kwenye
vyumba vichache ambavyo vilikuwa havijafungwa eneo hilo
kabla ya asubuhi kuambia tukio hilo la
kuuwawa kwake .
Johari Ngeng’ena mjumbe wa serikali
ya mtaa wa Kijiweni alisema kuwa mauwaji hayo ni ya
kwanza kwa mwaka huu na kuwa ila tukio hilo ni la
kinyama zaidi na limewasikitisha wananchi wa
mtaa huo .
Hata hivyo alisema kuwa kutokana
na tuko hilo wanampango wa kukaa
nchini ili kuangalia uwezekano wa
kuanzisha ulinzi wa jadi (sungusungu) pia kuwataka wafanyabiara
wa pombe katika eneo hilo kuwa na muda mzuri wa
kufunga na wale waliolima mahindi
mitaani basi kupewa taratibu
za manispaa za kuacha kulima mahindi mitaani
kwani mwili wa marehemu huyo umetupwa kwenye mahindi .
Beth Mdeta ambae ni muuzaji wa chumba ambacho nje
mauwaji hayo yalifanyika alisema kuwa kwa
upande wake alifunga mapema na kumuacha
Mdota akiwa kwenye katika maeneo
ya klabu hicho na sio ndani ya chumba chake
na kuwa amesikitishwa na kusikia mauwaji hayo yamefayika nje
ya chumba chake .
“ Mimi nilipigiwa simu
asubuhi na majirani zangu wakinieleza kuwa nje
ya chumba change kuna mauwaji yamefanyika maana
kuna damu nyingi na baadhi ya vitu kama mabaki
ya nguo yakiwa yametelekezwa nje eneo lenye
damu nyingi “
Mwenyekiti wa Klabu hicho Nicolina Mapunda
alisema kwa upande wake marehemu hamfahamu
kabisa na hata huo usiku ambao watu wanadai walimuona
eneo hilo kwa upande wake hakubahatika kukutana nae zaidi
ya kupigiwa simu majira ya saa 2 asubuhi .
Alisema kuwa yeye amekuwa
akifanya kazi ndani ya klabu hicho na
wafanyabiashara wenzake walimwita na
kumuonesha damu zilizotapakaa eneo hilo
japo alisema utaratibu wa klabu hicho kufungwa
ni saa 5 usiku ila siku hiyo yeye aliondoka
mapema zaidi .
Mwili wa marehemu huyo
ulikutwa ukiwa umechinjwa shingo na kitu
chenye ncha kali huku viatu vyake pamoja na
radio yake vikiwa vimeporwa na wauwaji hao
na mifuko ya suruali ikiwa nje kwa maana
ya pesa alizokuwa nazo kusachiwa na
wauwaji hao huku mkononi akiwa ameshikilia
rozari yake.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Juma
Bwire amethibitisha kutokea kwa tukio
hilo kuwa lilitokea majira ya saa10;20 alfajiri
na kuwa jeshi la polisi linaendelea kuwasaka watuhumiwa
wa mauwaji hayo
Comments
Post a Comment