![]() |
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mbwana Saleh Mhando akizungumza na waadishi wa habari ofisini kwake huku akihimiza wananchi kujikinga na ugonjwa wa COVID 19 pamoja na EBOLA. |
Na George Mwigulu,Tanganyika.
Wananchi wa Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi wametakiwa kuendelea
kuchukua hatua madhubuti za kupambana na kujikinga na ugonjwa wa COVID 19
pamoja na Ebola wawapo sehemu za mikusanyiko hususani minadani.
Hayo aliyasema Mkuu wa wilaya ya hiyo
Mbwana Saleh Mhando wakati akizungumza na Wanahabari ofisi kwake katika kata ya
Ifukutwa ambapo aliwataka wakazi hao kuwa waangalifu pamoja na kuchukua tahadhari kubwa wakati huu ugonjwa
wa corona unapoendelea kuenea hapa nchini.
Mkuu wa wilaya hiyo alieleza kuwa
kutokana na wilaya ya Tanganyika kupakana na nchi ya DRC Congo ambayo
imeshuhudiwa pia na maambukizi ya COVID
19 pamoja na ugonjwa wa Ebola.Hatua madhubuti zinatakiwa kuchukuliwa na
wananchi za kujikinga pasipo kuiachia jukumu hilo pekee serikali yao.
Mhando amefafanua kuwa hadi sasa
kunawageni pekee watatu kutoka nchi ya DRC Congo ambao wote kwa pamoja
wamehifadhiwa kwenye kituo cha Afya Karema kwa uagalizi wa kitabibu (Karatini)wa
siku kumi na nne.
Philipo Mihayo ambaye ni Afisa
Mazingira na Msimamizi wa kituo cha ukaguzi wa wageni wanao ingia kutoka Mkoa
wa Kigoma na maeneo ya Mwambao wa Ziwa Tanganyika amewataka wasafiri kuendelea
kuchukua hatua za kujikinga wawapo safarini
ikiwa pamoja na kunawa mikono na kutogusana.
Pamoja na hayo Philipo amewapongeza
wasafiri wote kwa kuwa na hamasa ya kujilinda kwa kunawa mikono kwa maji safi
na sabuni bila kushurutishwa kwa mguvu katika maeneo yote yaliyotengwa kwa
ukaguzi.
Elias Athony ambaye ni msafiri kutoka
Mkoa wa Kigoma kwenda Mpanda aliyeshuka kwenye kizuizi cha Kabungu kutii agizo la serikali la kunawa mikono na kupimwa joto lake la mwili
ameishukuru serikali ya wilaya ya Tanganyika kwa namna walivyojipanga kudhibiti
COVID 19.
Vile vile Elias ameiomba serikali
kuzidi kuchukua hatua zaidi za kuwaelimisha wananchi madhara yatokanayo na
COVID 19 jinsi ambavyo janga hilo la dunia linaweza kuathiri uchumi wao na
taifa kwa ujumla.
Esther Charles ambaye naye ni msafiri
aliye tii agizo la serikali alisema kuwa watu wasijisahau kujilinda na magonjwa
mengine ambayo ni hatari zaidi kama vile UKIMWI na EBOLA kwani kupambana pekee
na COVID 19 hakutasaidia kama kuna vifo vitazidi kushuhudiwa vya magonjwa hayo.
Aidha ameiomba serikali kutumia njia
hiyo hiyo ambayo wanaitumia kuhamasisha wananchi kujilinda na COVID 19 pia
waitumie katika kuelimisha wananchi kujilinda na magonjwa mengine.
Comments
Post a Comment