Na Mwandishi Wetu.
Katavi.
MTU
mmoja Mkazi wa Mtaa wa Mpanda Hotel katika Manispaa ya Mpanda
Mkoa wa Katavi aliyejulikana kwa jina la Paulo Chundu amekufa hapo hapo baada ya kupigwa na radi
akiwa anaaendesha pikipiki wakati akitokea kwenye shamba la mpunga .
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Benjamin Kuzaga aliwaambia wandishi wa habari
kuwa tukio la kifo cha marehemu huyo lilitokea hapo juzi majira ya saa
12 jioni katika eneo la Kalilankuluku Tarafa ya Kabungu Wilaya ya
Tanganyika .
Kuzaga
alieleza kuwa kabla ya tukio hilo marehemu huyo alikuwa ameaga nyumbani kwake
kuwa anapeleka chakula kwenye shamba lake la mpunga kwa ajiri ya
chakula cha vibarua waliokuwa wakifanya kazi kwenye shamba hilo .
Baada
ya kuwa ameaga nyumbani kwake marehemu huyo alipakia chakula hicho kwenye
pikipiki yake na kuelekea kwenye shamba hilo la mbuga ya mpunga lililoko
katika Kijiji cha Ikaka na alifika salama kwenye shamba hilo .
Kamanda
Kuzaga alieleza kuwa baada ya kuwa amefikisha chakula hicho na kukagua hali ya
maendeleo ya mbuga hiyo ya mpunga marehemu aliwaaga vibarua
waliokuwa wakifanya kazi na kuanza safari yake ya kurejea nyumbani kwake katika
Mtaa wa Mpanda Hotel.
Wakati
akiwa anaondoka kulikuwa na dalili za mvua kutaka kunyesha hata hivyo
hari hiyo haikumfanya ashindwe kuendelea na safari yake ndipo wakati alikuwa
amefika kwenye eneo la Kalilankulukulu alipigwa na radi wakati akiwa anaendesha
pikipiki na kufa hapo hapo .
Alisema
baada ya kuwa amepigwa na radi hiyo hadi kufa wananchi waliokuwa wanapita
kwenye eneo hilo la barabara hiyo inayotoka Mpanda Mjini kwenda Tarafa ya
Karema waliuona mwili huu wa marehemu ukiwa kati kati ya barabara huku pikipiki
yake ikiwa ipo pembeni yake .
Wananchi
hao waliweza kutowa taarifa kwa jeshi la Polisi ambao walifika kwenye
eneo hilo na kisha waliuchukuwa mwili wa marehemu na kuupeleka kwenye chumba
cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Katavi .
Kamanda Kuzaga alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha
kuhifadhi maiti katika hospitali hiyo na baada ya uchunguzi utakabidhiwa kwa
ndugu zake kwa ajiri ya mazishi aliwaondoa mashaka ndugu wa
marehemu kuwa kifo hicho kimetokana na radi ya mpango wa
Mungu na wala wasifikilie tofauti na hivyo .
Comments
Post a Comment