Mtaalam wa Usalama Mtandao na Uchunguzi wa Kidijitali, Bw. Yusuph Kileo akiwasilisha mada ya kuwajengea uelewa juu ya Elimu ya Usalama Mtandao wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jangwani Oktoba 12, 2022, jijini Dar es Salaam. Matukio mbalimbali katika picha wakati wa mafunzo ya elimu ya Usalama Mtandao katika Shule ya Sekondari ya Jangwani, Oktoba 12, 2022 jijini Dar es Salaam. ********************************************* Na Mwandishi Wetu,Dar Es Salaam. VIJANA na wanafunzi ni kundi lenye hatari kubwa ya kukumbwa na uhalifu wa mtandaoni kwa sababu ndio kundi lenye matumizi makubwa ya mtandao kwa ajili ya kufanya utafiti wa masomo, kununua vitu mtandaoni pamoja na matumizi ya mitandao ya kijamii kama twitter, whatsapp, intagram, tiktok n.k. Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari katika kuadhimisha mwezi wa kujenga uelewa kuhusu usalama mtandao unaoadhimishwa mwezi oktoba kila mwaka duniani pote imewafikia wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya wasichana ya Jangwani na ...