Na Castus Bhusolo,Site Blog-Mbeya.
*********************************
VIONGOZI wa vyama vya Wafanyakazi nchini wameombwa kuleta wafanyakazi wao katika chuo cha wafanyakazi OTU kilichoko mkoani Mbeya ili kupewa elimu itakayowasaidia kuondokana na migogoro ndani ya Vyama.
Ameyasema hayo Rais wa shirikisho la Vyama vya wafanyakazi nchini TUCTA Tumain Nyamhokya wakati akifunga mafunzo maalumu yaliyotolewa kwa wafanyakazi.
"Nawashukuru sana kwa ushirikiano wenu katika semina hii, Mmejifunza muundo wa vyama vyetu vya wafanyakazi, chati ya uongozi katika vyama vyetu lakini pia mmejifunza majukumu yenu kama wajumbe wa kamati tendaji ya Taifa ya chama cha wafanyakazi TALWGU ninaamini elimu hii mtaitumia vyema kwa manufaa ya chama na wafanyakazi kwa ujumla"
"Chuo hiki cha wafanyakazi Mbeya kilichangiwa na wafanyakazi wote nchi nzima wako waliokatwa kwenye mishahara yao na chuo hiki kikajengwa kimejengwa mwaka 1974-1975, 1976 kikaanza kutoa mafunzo nitoe wito kwa waajiri na viongozi wa vyama waleteni wafanyakazi katika chuo hiki ili wapate elimu Stahiki"
Makam Mwenyekiti wa TALWGU, Ronward Mwasuya ameeleza mafunzo wanayopewa viongozi yanawanufaisha kwakuwa mbali na kutanua wigo wa fikra na maarifa inawasaidia pia kujua namna kuwasimamia wafanyakazi katika haki zao.
"Ili uwe kiongozi bora unatakiwa kujua ni nini ukifanye kwa wanachama wako kwahiyo viongozi wanapoletwa kupatiwa elimu inawasaidia na kuwalahisishia usimamizi na utendaji katika kazi zao"
Mjumbe wa kamati ya utendaji Taifa Rehema Omary Kabanda amesema baada ya mafunzo haya sasa yuko tayari kwenda kuwaelimisha wafanyakazi juu ya haki na wajibu wao wanaotakiwa kufanya ikiwemo wajibu wa kustaafu nankukumbushara baadhi ya taratibu na misingibya maadili katika kazi.
Akizungumzia ubora wa chuo cha wafanyakazi Mbeya Mkuu wa Chuo hicho Ezron Kaya amesema jitihada za kutoa elimu kwa viongozi wa wafanyakazi zinaendelea hawana mashaka kwakuwa chuo hicho ni cha muda mrefu na kimewanoa vionvozi wengi.
"Mimi niseme Waajiri wasione shaka kuwaleta wafanyakazi wao kupewa elimu,chuo hiki kimejitosheleza na gharama zake ni za kawaida mfano kwa mtu mmoja ni Laki5 wiki nzima au siku tano na hapo unahudumiwa kila kitu na elimu unayopata ni ya uhakika! Sasa kwanini viongozi wasije kunolewa hapa!!?"
MWISHO.
Comments
Post a Comment