![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjhjP4FTRGMCdjRSEz5ZNjqKbleuc5LnKR2FDsaOtmV0Dqt3gDOEeSbBjckpGpvg-U-9y8xQ5XH_pKNn6VG3CKz8xBnzwBpbHy7gsaHA0a9WmnmLLqVSYAKe56L-pE3OQqcYO8T2n879QY7So9Y2u_sbh-iP3HivW2m0jhrxJD1ubHaXHXZIuURiCpX/w640-h360/vlcsnap-2022-10-29-03h40m06s0.png)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgIx2qQHDUSB5ARoLlt3BpAWocArbYPjIwhwvw8ntrK15aANC_tCnM-3Xe4CFVGdyT010IyJ88Bay62IbRX_k8VXpK7hk-BH3oNEPVPwrDOriu52XwZqozK2HF_g_nyhoCFzP8ARhnAffFSpZDI3kawiSW6AT0Flx3aUJEpcmSoIinNs_dBDdodFk68/w640-h360/vlcsnap-2022-10-29-03h41m26s0.png)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiQb3lc3wnRNYeXb1plzpJQAFAptig1qsjJBSJleasAX9ABMnUUN6tO4Ga11wuDrrGFJlHWr3NeN0GAuavB_4Cia4RmlU6Kt6VqkB1sPs_AtPZ-umuiCca8f2w3zE4noP_hYk700U3XNS0k0Dt6Ngprt_mldNnSOS-Fqijxyk3FvpTKFO2tmOOiDyEb/w640-h360/vlcsnap-2022-10-29-03h41m06s0.png)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiCb17uWc_UwtJeC3baPqRYFWRBjTNXcU3iMjw1bEZncH6sA5j2v3tnoMBVkFVq7i-OwE702SPMyjQIbJy3X6Qn9iSgqyB0FVkpSdQ64RANomg-PahwaQNd9i94e_pZRH9DY1vNlaW3TNtXR-ew6YtAbQGtzedy_-2UCYNAuAkxiKLQp6S7C2yD0Nk5/w640-h360/vlcsnap-2022-10-29-03h40m39s0.png)
Mkuu wa Wilaya ya Mlele Filberto Sanga akizungumza wakati wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Oktoba 27,2022.
Na Aidan Felson, Site Blog-Katavi.
********************************************
IMEBAINISHWA kuwa,Migororo ya Ardhi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Mkoani Katavi inazidi kuongezeka kila siku,huku chanzo cha migogoro hiyo kikitajwa ni viongozi.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Filberto Sanga,wakati wa kikao cha Baraza la madiwani la halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe lililofanyika Oktoba 27,2022 katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri.
Sanga amesema wapo baadhi ya viongozi wasio waadilifu wanatumia nafasi zao kuwachochea wananchi kuvamia maeneo ikiwemo viongozi hao kuwatapeli Wananchi kutoa maeneo yao kwa madai ni kwa ajili ya matumizi ya Kijiji wakati sio kweli.
Akitolea mfano moja ya mgororo,DC Sanga amesema "Kulikuwa na suala kule Ukimbwamizi,suala la mnara wa Voda,ule mgogoro ni ujanja tu. Wale viongozi wangu wanaelea,baada ya voda kufika Serikali ya Kijiji kutafuta eneo, viongozi wangu walienda kumshawishi Mama mmoja,tunaliomba hili eneo tulitumie kwa kazi za Kijiji"
"Yule Mama bila kujua,akaridhia akawapa,baada ya kuwapa muda haukupita 2019/20 Vodacom wakaenda pale kusimika mnara. Yule Mama akawaambia kumbe mlikuwa mnanizunguka mnajua hili? Basi naomba na Mimi nipate kidogo,wakasema hapana hatukupi wewe umeshalitoa hili eneo"
Kufuatia hali hiyo, Serikali imeamua mama huyo arudishiwe eneo lake na mkataba utenguliwe asaini mama huyo.
Katika hatua nyingine,amewataka viongozi wote Wilayani humo kufanya maandalizi ya utekelezaji wa miradi ya mazingira mapema kwa kuotesha vitalu ili ifikapo mwakani suala hilo litekelezwe kikamilifu kama yalivyo maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Hata hivyo,Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe limewataka wananchi wote waliojenga eneo la mnada lililopo Kata ya Majimoto kubomoa haraka na kuondoka eneo hilo kabla Serikali haijaingilia kati.
"Halmashauri yetu kwa ujumla tuna changamoto kubwa sana ya migogoro ya Ardhi,na hususani kwenye maeneo ya Kasisi na pale kwenye eneo letu la Majimoto kwenye mnada,wananchi wanaendelea kuvamia"- Alisema Mwenyeketi wa Halmashauri hiyo,Sailas Irumba.
Aidha,amesisitiza elimu izidi kutolewa kwa Wananchi ili kunusuru hifadhi za Misitu.
MWISHO.
Comments
Post a Comment