Skip to main content

WAHANGA WA VYETI "FEKI" WARUDISHIWA TABASAMU.


Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA) na Makam M/kiti wa TALWGU  Tumaini Nyamhokya.




Na Castus Bhusolo,Site Blog-Mbeya.

***************************************************************

KUFUATIA taarifa ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu, Joyce Ndalichako ya kuutaarifu UMMA kwamba Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia maombi ya viongozi kuwalipa wale wafanyakazi waliopata shida ya vyeti Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA),Tumaini Nyamhokya amewaongoza wafanyakazi wengine kumpongeza Rais Samia kwa moyo wake wa kuwajali na kuwafuta machozi wafanyakazi walioondolewa kwenye mfumo wa ajira kwasababu ya changamoto ya Vyeti.


Nyamhokya ambaye pia ni Makam M/kiti wa TALWGU amesema wafanyakazi hao Walitoka ghafla lakini sasa wanakwenda kulipwa Stahiki zao kila mmoja kwa kadri ya kiwango alichoweka.

"Ni ukweli wa wazi kuwa waliumia kwakuwa hawa wenzetu walizoea makazinii hawakujua kama kuna siku wataondolewa kwenye mfumo walizoea malezi ya serikali nasi kama Viongozi tumehangaika  kuwasaidia na kuwasemea tangu tulipoingia madarakani mwaka 2016 lakini sasa leo wanaenda kupata faraja walioweka asilimia 5 watalipwa asilimia tano na walioweka asilimia 10 watalipwa hiyohiyo.

Aidha Nyamhokya ameongeza kuwa "Wakati ule waliondolewa wengi, wenzetu wenye elimu ya darasa la saba walirejeshwa lakini hawa waliokuwa na shida ya vyeti hawakurejeshwa kazini na hawakuwahi kulipwa chochote lakini siku ya leo (jana) naamini taarifa hii itarejesha tabasamu lao lililopotea muda mrefu.

Elizabeth Kalinga ambaye ni mmoja wa waathirika, amesema wakati anakumbwa na mkasa huo alikuwa Mtendaji wa Kata Iwambi kwa zaidi ya miaka 15 na wakati anapokea taarifa ya kusitishwa kazi alikuwa anaumwa.

"Wakati nakumbwa na hili nilikuwa nimeomba kustaafu maana umri ulikuwa unafika, mwezi wa pili niliomba na mwezi wa tatu nikakubaliwa na mchakato wote ulikamilika na fedha ziliingia lakini nilipozifuata nikaambiwa zimezuiliwa," alisema Elizabeth.

Tumaini Mbonamasabo ambaye ni Afisa TEHAMA halimashauri wilaya ya Babati amesema Serikali inekuwa ikifanya kazi kwa ukaribu na viongozi wa wafanyakazi kama utoaji elimu juu ya uadilifu na uwajibikaji katika kazi hivyo kitendo alichokifanya Rais Samia cha kuridhia kuwapatia Mafao wafanyakazi hao ni kudhihirisha ubinadamu na utu alionao.

Changamoto hii ya kubaini Vyeti feki na wale wenye elimu isiyokidhi viwango kwa wafanyakazi ilianza mwaka 2016 ambapo mpaka kufika sasa ni miaka saba wako waliorejeshwa kazini na wako walioondolewa mpaka kufika sasa.

MWISHO.

Comments

Popular posts from this blog

WAJASIRIAMALI MPANDA WAILILIA SERIKALI KUCHELEWA UPATIKANAJI WA VITAMBULISHO

Na Swaumu Katambo, Katavi W afanyabiashara wadogo   katika stendi ya mabasi M izengo P inda wameiomba S erikali kuharakisha ugawaji wa vitambulisho ili kuep u kana na adha ya kulipa ushuru wa H almashauri ambao una   gharama  kubwa. W akizungumza na Site Tv  wajasiriamali M jini M panda wame i lalamikia H almashauri ya M anispaa ya M panda kuwatoza ushuru pasipo kuwa na utaratibu wowote . Mkurugenzi wa M anispaa ya M panda M ichael N zyungu amesema kuwa adha hiyo imetokana na kuchele we shwa kwa vitambulisho na amewataka wajasiriamali kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki. Vitambulisho vya ujasiriamali vilianzishwa na serikali maalumu kwa kuwasaidia wafanya   biashara wadogo kutoa huduma bila bugdha yoyote . MWISHO

Tufanye mabadiliko ya kina kwenye mfumo wa elimu -Mbunge Rose Tweve

KANISA KATOLIKI PAROKIA YA INYONGA LAFANYA MISA MAALUMU KUMUOMBEA DKT MAGUFULI, DC JAMILA ASISITIZA KUMUENZI KWA VITENDO

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda  ambaye pia ni  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mlele  Mhe  Jamila Yusu ph akisisitiza jambo wakati  akizungumza kwenye Misa Maalumu katika Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Mkuu wa Wilaya ya Mpanda  ambaye pia ni  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mlele  Mhe  Jamila Yusu ph akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Kanisa katoliki Parokia ya inyonga mara baada ya kumalizika  Misa Maalumu ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Kiongozi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga Padri  Maricelo Butoyi akiongoza Misa Maalumu ya  kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Sehemu ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga wakifuatilia ibada Maalumu ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Sehemu ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga wakifuatilia ibada Maalumu ...