Skip to main content

VIJANA, WANAFUNZI NA HATARI YA KUFANYIWA UHALIFU MTANDAONI.

Mtaalam wa Usalama Mtandao na Uchunguzi wa Kidijitali, Bw. Yusuph Kileo akiwasilisha mada ya kuwajengea uelewa juu ya Elimu ya Usalama Mtandao wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jangwani Oktoba 12, 2022, jijini Dar es Salaam.



Matukio mbalimbali katika picha wakati wa mafunzo ya elimu ya Usalama Mtandao katika Shule ya Sekondari ya Jangwani, Oktoba 12, 2022 jijini Dar es Salaam.

*********************************************

Na Mwandishi Wetu,Dar Es Salaam.

VIJANA na wanafunzi ni kundi lenye hatari kubwa ya kukumbwa na uhalifu wa mtandaoni kwa sababu ndio kundi lenye matumizi makubwa ya mtandao kwa ajili ya kufanya utafiti wa masomo, kununua vitu mtandaoni pamoja na matumizi ya mitandao ya kijamii kama twitter, whatsapp, intagram, tiktok n.k.

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari katika kuadhimisha mwezi wa kujenga uelewa kuhusu usalama mtandao unaoadhimishwa mwezi oktoba kila mwaka duniani pote imewafikia wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya wasichana ya Jangwani na kutoa mafunzo ya kujenga uelewa kwa wanafunzi wa kidato cha tano na sita wapatao 250.

Akizungumza katika mafunzo hayo Oktoba 12, 2022 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Msaidizi wa Usalama Mtandao wa Wizara hiyo, Mhandisi Stephen Wangwe ametoa rai kwa wanafunzi hao kuwa makini kabla ya kuposti chochote ili kujikinga na uhalifu wa mtandaoni kama vile udhalilishaji, utapeli na udukuzi wa taarifa binafsi.

“Ni muhimu kuchukua tahadhali kwa kuacha tabia ya kuposti kila kitu mtandaoni na iwapo ikatokea umefanyiwa utapeli au viashiria vyovyote vya uhalifu wa mtandao inashauriwa kuripoti kituo cha polisi kilicho karibu kwa hatua stahiki kwa kuwa usalama wa mtandao huanza na mtu binafsi”, amesisitiza Mhandisi Wangwe

Mhandisi Wangwe ameongeza kuwa elimu ya usalama mtandao ni muhimu sana ili watumiaji wa mitandao waweze kujilinda na athari zinazokuja na kukua kwa teknolojia ambapo wahalifu na wadukuzi nao hutumia teknolojia hiyo hiyo kufanya uhalifu na kugusa maisha ya watumiaji kwa kuharibu taswira na dira ya maisha yao.

Naye Mtaalamu wa Masuala ya Usalama Mtandao na Uchunguzi wa Kidijiti wa African ICT Alliance (AfICTA) kutoka Tanzania, Bw. Yusuph Kileo amewataka wanafunzi na vijana kutumia mitandao kwa uadilifu na kuzingatia usiri wa taarifa binafsi, na kuhakikisha namba za siri za akaunti zao ni imara, ngumu kutabirika na hazifanani.

Mwalimu Salum Kilipamwambu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Jangwani amesema licha ya somo ya TEHAMA kufundishwa shuleni hapo kulikuwa na umuhimu mkubwa kwa wanafunzi hao kujengewa uelewa kuhusu matumizi salama ya mtandao na kuwashukuru wataalamu wa Wizara kufika shuleni hapo.

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi hao Bi. Anna Ngowi mwanafunzi wa kidato cha sita amekiri kuwa elimu ya usalama mtandao imewapa majibu mengi ya nini cha kufanya kujilinda na uhalifu mtandaoni na kuahidi watakuwa mabalozi wazuri kwa wanafunzi na vijana wenzao.

MWISHO.

Comments

Popular posts from this blog

WAJASIRIAMALI MPANDA WAILILIA SERIKALI KUCHELEWA UPATIKANAJI WA VITAMBULISHO

Na Swaumu Katambo, Katavi W afanyabiashara wadogo   katika stendi ya mabasi M izengo P inda wameiomba S erikali kuharakisha ugawaji wa vitambulisho ili kuep u kana na adha ya kulipa ushuru wa H almashauri ambao una   gharama  kubwa. W akizungumza na Site Tv  wajasiriamali M jini M panda wame i lalamikia H almashauri ya M anispaa ya M panda kuwatoza ushuru pasipo kuwa na utaratibu wowote . Mkurugenzi wa M anispaa ya M panda M ichael N zyungu amesema kuwa adha hiyo imetokana na kuchele we shwa kwa vitambulisho na amewataka wajasiriamali kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki. Vitambulisho vya ujasiriamali vilianzishwa na serikali maalumu kwa kuwasaidia wafanya   biashara wadogo kutoa huduma bila bugdha yoyote . MWISHO

Tufanye mabadiliko ya kina kwenye mfumo wa elimu -Mbunge Rose Tweve

KANISA KATOLIKI PAROKIA YA INYONGA LAFANYA MISA MAALUMU KUMUOMBEA DKT MAGUFULI, DC JAMILA ASISITIZA KUMUENZI KWA VITENDO

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda  ambaye pia ni  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mlele  Mhe  Jamila Yusu ph akisisitiza jambo wakati  akizungumza kwenye Misa Maalumu katika Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Mkuu wa Wilaya ya Mpanda  ambaye pia ni  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mlele  Mhe  Jamila Yusu ph akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Kanisa katoliki Parokia ya inyonga mara baada ya kumalizika  Misa Maalumu ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Kiongozi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga Padri  Maricelo Butoyi akiongoza Misa Maalumu ya  kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Sehemu ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga wakifuatilia ibada Maalumu ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Sehemu ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga wakifuatilia ibada Maalumu ...