Skip to main content

TANGANYIKA: WATU 32,000 WAPATA CHANJO YA UVIKO-19 NDANI YA SIKU SABA.

Sehemu ya Wananchi wa Luhafwe wakiwa wamejitokeza kupata chanjo ya UVIKO-19 leo Oktoba 31,2022.

Mratibu wa chanjo Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, Philip Mihayo.
Zawadi Dakika,Afisa miradi kutoka Taasisi ya Benjamini Mkapa

Shaban Juma,Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika.

Dokta Alex Mrema,Mganga Mkuu Wilaya ya Tanganyika.



Na Aidan Felson,Site Blog-Katavi.
******************************************

HALMASHAURI ya Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi kwa kushirikiana na Taasisi ya Benjamini Mkapa imefanikiwa ndani ya siku Saba kuwafikia na kuchanja Watu 32,000 wa chanjo ya kuzuia ugonjwa wa UVIKO-19 katika Halmashauri hiyo, kupitia kampeni ya uhamasishaji wa uchanjanji nyumba kwa nyumba ya siku Tisa.

Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la Kijiji cha Luhafwe sehemu iliyotengwa maalum kwa ajili ya utoaji chanjo,Mratibu wa chanjo Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, Philip Mihayo amesema idadi hiyo imefikiwa kutokana na hamasa na mbinu shirikishi iliyotumika kuwaelimisha Wananchi.

"Tulikuwa na asilimia kama 32 hivi kabla ya ujio wa wadau Taasisi ya Benjamini Mkapa. Imekuja kutupa hamasa kubwa kwa sababu tumetumia mbinu ya kuwaita viongozi wa dini, viongozi wa jamii,watu wa tiba asili,tumeahirikisha watu maalfu kwa sasa hivi mwitikio ni mkubwa sana"

Zawadi Dakika,Afisa miradi kutoka Taasisi ya Benjamini Mkapa amesema sababu za kuleta mradi huo katika Mkoa wa Katavi ni kutokana na kuwa ni moja ya Mkoa ambao uko nyuma kwa uchanjaji kutokana na hamasa kuwa chini.

Bi. Dakika amesema, kabla kampeni haijaanza Oktoba 24,2022 mkoa wa Katavi ulikuwa umechanja kwa asilimia 51 lakini ndani ya siku Saba baada ya zoezi hilo kuanza mkoa umefikia asilimia 85 ya uchanjaji.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, Shaban Juma,leo Oktoba 31,2022 amefika kujionea namna zoezi hilo linaendelea ambapo ameridhishwa na mwitikio wa Wananchi huku akiishukuru Taasisi ya Benjamini Mkapa kwa kujumuika nao katika kuhamasisha zoezi hilo.

Baadhi ya Wananchi James Fanuel na Mateso Masalu wakazi wa Luhafwe baada ya kuchanja wamesema,chanjo hiyo haiko kama walivyosikia taarifa za kupotosha kuwa ukichanja unapata madhara.

"Huo ni uongo kwa sababu kila mmoja ana fikra yake na huenda anayesema sio Daktari mwenye vigezo,na siamini kama Mama Samia (Rais) anaweza kukubali kututeketeza Wananchi wake"-Amesema James Fanuel.

Kwa upande wake Mganga mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika,Dkt. Alex Mrema amesema Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika inatarajia kuwafikia Wananchi 150,000.

Dkt. Mrema amewatoa hofu Wananchi kuwa chanjo hiyo ni salama na hakuna madhara yoyote hivyo kwa wale ambao bado hawajachanjwa wafike katika vituo vya afya kwa ajili ya kupatiwa chanjo ya UVIKO-19.

"Chanjo inayotolewa ni aina ja Jensen ambayo ni ya dozi moja. Ndugu Wananchi,niwahakikishie usalama wa chanjo ya UVIKO-19,chanjo hii ni salama."

Zoezi hilo la uchanjaji litaendelea katika vituo vya afya vya Halmashauri hiyo hata baada ya siku Tisa za kampeni ya uhamasishaji nyumba kwa nyumba kumalizika.

MWISHO.

Comments

Popular posts from this blog

Mkuu wa Mkoa wa Katavi akibidhiwa Ofisi,aelezwa Miradi ya kusimamia.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi,Mwanamvua Hoza Mrindoko wa kwanza Kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera wakati wa makabidhiano ya Ofisi. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi Beda Katani. Wakuu wa Wilaya,Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Rachel Kasanda. Na Mwandishi Wetu,Site Tv Mapema leo Mei 25,2021 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko,amekabidhiwa Ofisi na aliye kuwa Mkuu wa Mkoa huo Juma Zuberi Homera aliye hamishiwa Mkoani Mbeya kuwa Mkuu wa Mkoa. Katika makabidhiano hayo,Homera amemtajia Mkuu wa Mkoa wa Katavi miradi ambayo inatakiwa kusimamiwa hadi ikamilike ni pamoja na Bandari ya Karema,Hosipitali ya Rufaa Mkoa,Kiwanda cha Nguo,Jengo la Utawala pamoja na Umeme wa Gridi ya Taifa. Aidha,amesema Katavi ni Nyumbani hivyo atatoa ushirikiano kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi huku akiwakaribisha Viongozi na Wananchi kwa ujumla katika Mkoa wa Mbeya. "Kuna hili la Gridi ya Taifa ambalo linaendelea,kuna Kiwan...

Tabasamu hili kwa Wanafunzi,Nuru imewaka Juu yao/Mwekezaji afanya Jambo ...

Ajira Mpya Wakaribishwa Mlele, Full Kula Bata/Makubwa yaja