Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi akivalishwa Tuzo na Balozi wa Ufaransa Nchini Tanzania Mhe.Frederic Clavier kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Ufaransa Emmanuel Macron. Na,Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ametunukiwa Tuzo ya Juu ya Heshima inayofahamika kama “Legion d’ Honner” na Rais wa Jamhuri ya Ufaransa Emmanuel Macron kutokana na mchango wake mkubwa wakati akiwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa la Tanzania. Rais Dk. Mwinyi alitunukiwa Tuzo hiyo leo na Balozi wa Ufaransa Nchini Tanzania Mhe.Frederic Clavier kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Ufaransa Emmanuel Macron, tukio lililofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar ambapo Balozi huyo alihudhuria akiwa na ujumbe wake. Rais Dk. Mwinyi alitoa shukurani zake za dhati kwa Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwa kumtunukia Tuzo hiyo iliyotokana na kuthamini kwa dhati mchango wake mkubwa alioutoa wakati akiwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa...