Skip to main content

NAIBU WAZIRI APIGA MARUFUKU KURUBUNI WANANCHI MAENEO YA UJENZI WA MINARA.


Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew (katikati)
akizungumza katika eneo la ujenzi wa mnara wa TTCL katika kijiji cha Chang’ombe kilichopo
Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma wengine ni watendaji aliombatana nao na wananchi wa eneo
hilo.


Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew (wa pili kulia)
akipokea zawadi ya gunia la mahindi kutoka kwa wananchi wa Kijiji cha Njoge alipofika kukagua
ubora, uwezo na upatikanaji wa huduma ya mawasiliano katika baadhi ya maeneo ya Wilaya ya
Kongwa.


Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew (wa pili kulia)
akikagua kitabu cha mahudhurio kwenye kituo cha huduma za Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano
kilichopo katika Ofisi za TTCL Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma. Wa kwanza Kushoto ni Mkuu
wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Remedius Mwema Emmanuel.


Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew (wa pili kushoto)
alipotembelea Ofisi za Shirika la Posta Wilaya ya Kongwa na kukagua utoaji wa huduma za
Shirika hilo wakati wa ziara yake ya kukagua ubora, uwezo na upatikanaji wa huduma za
mawasiliano katiak Wilaya hiyo. Wa kwanza Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe.
Remedius Mwema Emmanuel.

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew akizungumzia na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka (Kulia) kabla ya kuanza ziara yake katika Wilaya ya Kongwa iliyopo katika Mkoa wa Dodoma kukagua ubora, uwezo wa miundombinu na upatikanaji wa huduma za mawasiliano.

Na Faraja Mpina, DODOMA

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Mathew amepiga marufuku tabia ya baadhi ya watendaji wa makampuni ya simu wasio waaminifu pamoja na washirika wao kuwarubuni wananchi kuuza maeneo yao kwa ajili ya ujenzi wa minara ya mawasiliano bila wao kujua kuwa wanauza kwa ajili ya ujenzi huo

Akiwa katika ziara yake ya kikazi Mkoani Dodoma katika Wilaya ya Kongwa Mhandisi Kundo amesema kuwa kuna malalamiko mengi kutoka kwa wananchi kurubuniwa kuuza maeneo yao lakini baada ya muda mfupi minara ya mawasiliano inajengwa katika maeneo hayo ambapo kodi ya ardhi ya eneo husika inaanza kulipwa kwa mmiliki mpya na mwananchi aliyeuza eneo lake kwa gharama ndogo hapati chochote

Ameongeza kuwa inafahamika kuwa kila mtu ana haki ya kisheria ya kumiliki eneo, kuuza na kupangisha eneo lake kwa kodi atakayoona inafaa lakini kinachofanyika katika baadhi ya maeneo ni wananchi kushawishiwa kuuza maeneo yao bila kujua kuwa ni eneo linalokuja kufanyiwa uwekezaji baada ya kufanyiwa utafiti na kuonekana linafaa kujengwa mnara wa mawasiliano

“Jukumu la Serikali ni kulinda maslahi ya wananchi hivyo naelekeza kila Mkurugenzi wa Halmashauri anapaswa kutambua umiliki wa eneo husika kabla ya kutoa kibali cha ujenzi wa mnara wowote ili kujiridhisha kama mmiliki wa eneo hilo anatambuliwa na Serikali ya kijiji husika”, alizungumza Mhandisi Kundo

Kwa upande wa malipo ya kodi ya ardhi kwenye maeneo yanayoenda kujengwa minara Mhandisi Kundo ameelekeza mikataba yote kufanyika kupitia ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kwasababu yeye ndiye mwenye wataalam wanaojua thamani na gharama za maeneo yaliyopo ndani ya halmashauri husika

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Remedius Mwema Emmanuel amesema kuwa katika Wilaya ya Kongwa kumekuwa na malalamiko mengi na migogoro kutoka kwa wananchi kuhusu kurubuniwa kuuza maeneo yao na wakati mwingine wenyeviti wa vijiji wamekuwa wakitumika kuhamasisha wananchi

Ameongeza kuwa katika kata ya Nghumbi kijiji cha Mbagirwa kuna mnara wa mawasiliano lakini mmiliki wa eneo husika hajulikani na Serikali ya kijiji haipati kodi yeyote kutoka katika mnara huo

Aidha, katika ziara yake ya kikazi katika Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Naibu Waziri huyo ameendelea kupokea na kuzitafutia ufumbuzi changamoto mbalimbali zinazogusa Sekta ya Mawasiliano ikiwa ni pamoja na kupokea mahitaji ya wananchi ya kuboreshewa huduma ya mawasiliano ya simu na intaneti

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Comments

Popular posts from this blog

Mkuu wa Mkoa wa Katavi akibidhiwa Ofisi,aelezwa Miradi ya kusimamia.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi,Mwanamvua Hoza Mrindoko wa kwanza Kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera wakati wa makabidhiano ya Ofisi. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi Beda Katani. Wakuu wa Wilaya,Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Rachel Kasanda. Na Mwandishi Wetu,Site Tv Mapema leo Mei 25,2021 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko,amekabidhiwa Ofisi na aliye kuwa Mkuu wa Mkoa huo Juma Zuberi Homera aliye hamishiwa Mkoani Mbeya kuwa Mkuu wa Mkoa. Katika makabidhiano hayo,Homera amemtajia Mkuu wa Mkoa wa Katavi miradi ambayo inatakiwa kusimamiwa hadi ikamilike ni pamoja na Bandari ya Karema,Hosipitali ya Rufaa Mkoa,Kiwanda cha Nguo,Jengo la Utawala pamoja na Umeme wa Gridi ya Taifa. Aidha,amesema Katavi ni Nyumbani hivyo atatoa ushirikiano kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi huku akiwakaribisha Viongozi na Wananchi kwa ujumla katika Mkoa wa Mbeya. "Kuna hili la Gridi ya Taifa ambalo linaendelea,kuna Kiwan...

Tabasamu hili kwa Wanafunzi,Nuru imewaka Juu yao/Mwekezaji afanya Jambo ...

Ajira Mpya Wakaribishwa Mlele, Full Kula Bata/Makubwa yaja