Skip to main content

TTCL YATAKIWA KUONESHA USHINDANI KATIKA SOKO LA MAWASILIANO NCHINI.

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew (Aliyesimama
katikati kwenye Chuma) akizungumza katika eneo la ujenzi wa mnara wa TTCL katika kijiji cha
Masenge Mamiwa Wilaya ya Gairo Morogoro wengine ni watendaji aliombatana nao na
wananchi wa eneo hilo.

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew (wa kwanza
kulia) akizungumza katika eneo la ujenzi wa mnara wa TTCL katika kijiji cha Masenge Mamiwa
Wilaya ya Gairo Morogoro wakati wa Ziara yake ya kukagua miundombinu na upatikanaji wa
huduma ya mawasiliano katika Mkoa huo.


Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew (wa pili kulia
mstari wa mbele) akizungumza wakati wa ziara yake katika mnara wa mawasiliano wa TTCL
uliopo katika Kijiji cha Kiganira Morogoro vijijini. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya ya
MorogoroVijijini Mhe. Albert Msando.


Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew akizungumza
wakati wa ziara yake ya kukagua miundombinu na upatikanaji wa huduma ya mawasiliano katika
kata ya Chakware iliyopo Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro.


Na Mwandishi wetu, MOROGORO

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limetakiwa kuonesha ushindani katika soko la mawasiliano nchini kwa kupanua wigo wa mtandao wake pamoja na kuboresha upatikanaji wa huduma zake za laini za simu, vocha, T- Pesa katika maeneo ya mijini na vijijini ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma muhimu na ya msingi ya mawasiliano ya sauti na data

Akiwa katika ziara ya kukagua miundombinu ya mawasiliano na hali ya upatikanaji wa huduma ya mawasiliano katika Mkoa wa Morogoro Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Mathew amesema kuwa katika ziara alizofanya

Mikoa ya Mtwara, Kilimanjaro na Tanga amekutana na changamoto za upatikanaji wa huduma za Shirika hilo wakati wananchi wanahitaji kutumia mtandao wa TTCL

Amesema kuwa tabia za wateja zinaenda sambamba na mabadiliko ya teknolojia kwa mfano matumizi ya data kuongezeka kwasababu ya mitandao ya kijamii na programu tumizi zinazotoa huduma za kijamii hivyo katika zama hizi za kidijitali Shirika la TTCL linatakiwa kwenda sambamba na mabadiliko ya tabia za wateja ili kuakisi mahitaji yao

“Shirika la TTCL mnatakiwa kuboresha na kuongeza wigo wa upatikanaji wa mtandao wenu na huduma zake badala ya kuweka uwekezaji mkubwa kwenye promosheni halafu wateja wakija hawapati huduma wanazostahili kuzipata”, alizungumza Mhandisi Kundo

Aliongeza kuwa ni kazi kubwa kumrejesha mteja ambaye Shirika litampoteza kutokana na kukosekana kwa huduma alizotarajia kuzipata hivyo kulitaka Shirika hilo kuboresha miundombinu yake ili huduma zake ziwe na uwezo unaokidhi mahitaji

“TTCL kuna Minara imejengwa na imekamilika lakini haijawashwa nendeni mkaiwashe,na ile ambayo ilikuwa tayari ipo kwenye mpango wa kujengwa ijengwe,inayotakiwa kuongezewa uwezo iongezewe, kwasababu hili ni Shirika la umma hivyo mnatakiwa kuwafikia wananchi katika maeneo yote hadi yale yasiyokuwa na mvuto wa biashara”,alizungumza Mhandisi Kundo

Aidha,amezungumzia huduma ya intaneti yenye kasi kuwa ni huduma ya msingi yenye mchango mkubwa wa kuipeleka nchi kwenye uchumi wa kidijitali na kufanyika kwa biashara mtandao ambapo ni wajibu wa Serikali kupitia taasisi za mawasiliano kuhakikisha wananchi wake katika maeneo yote wanapata na kutumia huduma ya intaneti.

Kwa upande wa wananchi waliojitokeza katika miradi ya minara ya mawasiliano ya TTCL iliyopitiwa wakati wa ziara ya Naibu Waziri huyo wamesema kuwa wao wanahitaji kurudi nyumbani kwa sababu wanaambiwa kumenoga kama kauli mbiu ya Shirika hilo inavyosema “Rudi Nyumbani Kumenoga” hivyo wameomba kuboreshewa uwezo na ubora wa mtandao huo pamoja na huduma za vocha, laini za simu na T-Pesa kwasababu katika maeneo mengi hazipatikani na wakati mwingine wanatembea umbali mrefu kutafuta huduma hizo.

Katika ziara hiyo Naibu Waziri aliambatana na watendaji wa Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo ikiwemo watendaji kutoka Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) ambapo walipokea maelekezo ya Naibu Waziri kuhusu kufuata utaratibu wa ujenzi wa miundombinu ya mawasiliano katika vipengele vya ubora, uwezo, vibali vya ujenzi, mikataba ya ujenzi na ulinzi na mahitaji ya wananchi kwa ujumla wake na kuahidi kuwa Shirika litafanyia kazi maelekezo hayo kwa muda muafaka

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Comments

Popular posts from this blog

WAJASIRIAMALI MPANDA WAILILIA SERIKALI KUCHELEWA UPATIKANAJI WA VITAMBULISHO

Na Swaumu Katambo, Katavi W afanyabiashara wadogo   katika stendi ya mabasi M izengo P inda wameiomba S erikali kuharakisha ugawaji wa vitambulisho ili kuep u kana na adha ya kulipa ushuru wa H almashauri ambao una   gharama  kubwa. W akizungumza na Site Tv  wajasiriamali M jini M panda wame i lalamikia H almashauri ya M anispaa ya M panda kuwatoza ushuru pasipo kuwa na utaratibu wowote . Mkurugenzi wa M anispaa ya M panda M ichael N zyungu amesema kuwa adha hiyo imetokana na kuchele we shwa kwa vitambulisho na amewataka wajasiriamali kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki. Vitambulisho vya ujasiriamali vilianzishwa na serikali maalumu kwa kuwasaidia wafanya   biashara wadogo kutoa huduma bila bugdha yoyote . MWISHO

Tufanye mabadiliko ya kina kwenye mfumo wa elimu -Mbunge Rose Tweve

KANISA KATOLIKI PAROKIA YA INYONGA LAFANYA MISA MAALUMU KUMUOMBEA DKT MAGUFULI, DC JAMILA ASISITIZA KUMUENZI KWA VITENDO

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda  ambaye pia ni  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mlele  Mhe  Jamila Yusu ph akisisitiza jambo wakati  akizungumza kwenye Misa Maalumu katika Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Mkuu wa Wilaya ya Mpanda  ambaye pia ni  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mlele  Mhe  Jamila Yusu ph akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Kanisa katoliki Parokia ya inyonga mara baada ya kumalizika  Misa Maalumu ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Kiongozi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga Padri  Maricelo Butoyi akiongoza Misa Maalumu ya  kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Sehemu ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga wakifuatilia ibada Maalumu ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Sehemu ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga wakifuatilia ibada Maalumu ...