MKOA WA KATAVI UMEJIPANGA KULETA MAPINDUZI YA KIUCHUMI KWA KUONGEZA VIWANDA,KUKUZA SEKTA YA MADINI NA KILIMO.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh Juma Zuberi Homera. Na Swaum Katambo Mpanda-Katavi Kuelekea mwishoni mwa Mwaka wa fedha,Mkoa wa Katavi umejiandaa kuleta mapinduzi makubwa ya Kiuchumi ikiwemo kuongeza Viwanda,kuongeza Vyuo,kukuza sekta ya Madini,Kilimo na Umeme Vijijini. Akitoa mwelekeo wa Mkoa,Mkuu wa Mkoa Mh. Juma Zuberi Homera katika kikao na Waandishi wa Habari kilichofanyika Ofisini kwake Juni 24,2020 amezungumzia mwenendo wa Soko la Madini na mikakati ya kuongeza kasi ya ununuzi na uuzaji wa Madini. Kuhusu Madini Mh Homera alisema,toka Soko la Madini lianze Mei,2019 hadi Juni 2020 Mkoa umefikisha Kilogra 254 za Madini na Gram 734 zenye thamani zaidi ya Tsh. Bilioni 24 ambapo kupitia soko la Madini Mkoa umeshakusanya kiasi cha Tsh. Bilioni 1.7 huku tozo za huduma kutoka katika Sekta ya Madini ikichangia zaidi ya Milioni 66. Alisema matarajio ni kuhakikisha ongezeko la ununuzi na uuzaji wa madini,na Serikali imeshapata eneo la uchimbaji Madini la zaidi ya Hekta 1901 kutoka ...