Skip to main content

Posts

Showing posts from April, 2020

TANGA YAJIDHATITI NA MAPAMBANO DHIDI YA COVID 19

  Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigella akipokea Matanki matano kutoka wa wadau wa mapambano ya COVID 19 jijini humo Na Mwandishi Wetu       Tanga MKUU wa Mkoa wa Tanga Martin Shigella amepokea vifaa vya kujikinga na ugongwa wa COVID 19 ikiwa sambamba na kuwataka wafanyabiashara wengine kuguswa na kuchangia vifaa vya usafi ili kuhakikisha wanadhibiti na kuchukua hatadhati za kujikinga na ugonjwa huo. Kauli hiyo ameitoa wakati akipokea msaada wa mataki matano ya ujazwa wa lita mia tano kila moja kutoka kampuni ya vifaa vya ujenzi ya Hussain Plastic Industry ya jijini hapa. Shigella amasema bado kunauhitaji mkubwa wa vifaa kwa ajili ya kusabazwa   kwenye maeneo mengine ya mkoani Tanga ili wananchi waweze kujikinga na COVID 19 kupitia kunawa mikono kwa maji safi yanyotiririka . Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Hussein Yusuph amesema kuwa wameamua kutoa msaada huo ili kuuga juhudi juhudiza serikali katika mapambano katika kukabili...

WALTEREED WATOA MSAADA WA VIFAA TIBA KATAVI KUPAMBANA NA COVID 19

  Mkuu wa Mkoa wa Katavi Comrade Juma Homera wa kwanza kutoka kulia akikabidhiwa box ya vifaa kutoka shirika la WalterReed na Dkt Shabain Ndama wa kwanza kutoka kushoto kwenye picha. Na Mwandishi Wetu        Katavi Serikali ya Mkoa wa Katavi katika kuendelea kukabiliana na ugonjwa wa   COVID-19 imefanikiwa kupokea vifaa   tiba kutoka shirika la WalteReed vyenye thamani ya milioni ishirini na tano ili kuhakikisha mkoa huo haupatikani na mgonjwa hata mmoja wa virusi hivyo. Mkoa huo hapo awali ulikabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba wa vitendea kazi kama vile Scaner kwenye baadhi   ya vituo vya vizuizi kwenye mipaka yake ya Burudi   na DRC Congo. Akikabidhi vifaa hivyo Meneja Mradi WalterReed (HJFMRI) Mkoa wa   Katavi   Dkt Shabain Ndama mbele ya   Mkuu wa Mkoa huo Juma Homera   amesema kuwa vifaa hivyo vimetolewa ili kuendelea kuthibiti maambukizi   ya ugonjwa wa COVID 19. ...

JESHI LA POLISI KATAVI LAPEWA MASAA 48 KUMPELEKA RAIA WA CHINA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA KUSHINDWA KUNAWA MIKONO

  Mkuu wa Mkoa wa Katavi comrade Juma Homerawa kwanza kutoka kulia kwenye picha. Na Mwandishi Wetu        Katavi.  Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Homera ametowa saa 48 kwa jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi kumfikisha Mahakamani Raia wa Nchi ya China aitwaye  Lin  Guosong (34) mfabiashara Mkazi wa Mtaa wa Majengo Manispaa ya Sumbawanga ambae alikamatwa kwa tuhuma za  kukataa kutii mashariti ya kujikinga na ugonjwa wa Corona  COVID -19.     Homera alitowa maagizo hayo hapo  (leo) jana mbele ya wandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa vifaa tiba vya kujikinga na ugonjwa wa COVID -19.  Vifaa hivyo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 25 vilitolewa na  shirika la Walter Reed walivyokabidhi msaada kwa Mkuu wa Mkoa na Meneja wa mradi Walter Reed (HJFMRI) Dkt  Shaban  Ndama . Alisema  Raia huyo wa Nchi ya China alikamatwa na jeshi la polisi ka...

DC MHANDO ATANGAZA VITUO 58 VYA KUNUNULIA MAZAO YA NAFAKA TANGANYIKA.

  Add caption Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Saleh Mhando akizungumza na waadishi wa habari ofisini kwake kartika kijiji cha Ifukutwa akitaja jumla ya vituyo 58 vya kununulia mazao mbalimbali ikiwamo pia kuwahimiza wakulima kutumia mfumo wa stakabadhi gharani. Na Mwandishi Wetu       Tanganyika. Wakulima wa mazao ya chakula na biashara wa Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi wameshauriwa kuuza mazao yao kupitia mfumo wa stakabadhi gharani pamoja na maeneo ya vituo maalumu yaliyotengwa kibiashara na Wilaya hiyo ili kunufaika na uzalishaji wao.   Akizungumza jana ofsini kwake katika Kata ya Ifukutwa Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Saleh Mhando   aliweka wazi kuwa utaratibu wa mfumo wa stakabadhi gharani na kuweka vituo maalumu vya kibiashara (soko) wameamua kuanzisha ili kuhakikisha mkulima anaweza kunufaika. Mhando aliainisha baadhi ya mazao ambayo yatatumika kuuzwa kupitia stakabadhi gharani ni Alzeti,Pamba,Kahawa...