Na Mwandishi Wetu
Tanganyika.
Wakulima wa mazao ya chakula na
biashara wa Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi wameshauriwa kuuza mazao yao
kupitia mfumo wa stakabadhi gharani pamoja na maeneo ya vituo maalumu
yaliyotengwa kibiashara na Wilaya hiyo ili kunufaika na uzalishaji wao.
Akizungumza jana ofsini kwake katika
Kata ya Ifukutwa Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Saleh Mhando aliweka wazi kuwa utaratibu wa mfumo wa
stakabadhi gharani na kuweka vituo maalumu vya kibiashara (soko) wameamua kuanzisha
ili kuhakikisha mkulima anaweza kunufaika.
Mhando aliainisha baadhi ya mazao
ambayo yatatumika kuuzwa kupitia stakabadhi gharani ni Alzeti,Pamba,Kahawa,Korosho,Tumbaku
na ufuta huku mazao ya
Mahidi,Karanga,Mpunga,Mhongo,Mtama pamoja na viazi
vitanunuliwa katika vituo maalumu vilivyowekwa na Wilaya hiyo.
Katika kuhakikisha ufanisi wa
utaratibu huo uliowekwa unazingatiwa Mkuu wa wilaya hiyo alisema kuwa Mkulima
yeyote yule hataruhusiwa kuuza mazao yake nje ya maeneo ya vituo vilivyotengwa
sambamba na wanunuzi hawataruhusiwa kununua bila kuzingatia utaratibu huo.
“…utaratibu uliokuwa ukitumika hapo
awali wa kumwita mfanyabiashara nyumbani au shambani na kupima mazao umeisha
kuazia leo hii,Na yeyote atakaye bainika kufanya hivyo hatua kali zitachukuliwa
dhidi yake”Alisisitiza Mhado.
Utaratibu mwingine utakao tumika ni
mazao yote kuuzwa kwa kutumia mizani zilizozibitishwa na wakala wa vipimo ili
kuepusha mkulima kuuibiwa mazao yake.Ikiwa pamoja na kupiga marufuku utumiaji wa ndoo aina ya Mozambique ambazo
husababisha hasara kwa mkulima.
Mkuu wa wilaya hiyo akitaja vituo
vitakavyo tumika kununulia mzao hayo ni jumla ya kata zote za wilaya ya
Tanganyika zitatumika na kuwa na jumla ya vituo 58 huku akisisitiza kuwa
hapatakuwa na vituo zaidi ya viwili kwenye eneo moja bali kutakuwa na kituo
kimoja ambacho wanunuzi wote watatumia kununulia mazao hayo.
Aidha alisema kuwa wafanyabiashara
wote hawataweza kuruhusiwa kununua mazao bila kuwa na kibali cha biashara pamoja
na kibali cha ununuzi kutoka ofisi ya Mkurugenzi huku kutakuwa na kibali
maalumu cha kusafirishia mazao yaliyonunuliwa kutoka ofisi ya Mkuu wa wilaya
isipokuwa kwa watu wale watakao kuwa wanasafirisha mazao chini ya tani moja.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya
Tanganyika John Rumuri alisema kuwa kunafaida nyingi zaidi za kutumia mfumo wa
stakabadhi gharani pamoja na kutengwa kwa vituo maalumu kuwa vimelenga
kumkomboa mkulima ili aweze kunufaika na kilimo chake.
Rumuri alifafanua kuwa utaratibu wa
stakabadhi gharani umewekwa kisheria hivyo hawataweza kumfumbia macho mtu
yeyote atakaye kiuka utaratibu huo wa kisheria .
Aliongeza kuwa kunaumuhimu watu
kuufuata ili kuisaidia serikali kupata takwimu uzalishaji wa mazao hao pamoja
na kaisi kilichouzwa na kubaki na kusaidia ukusanyaji wa matapo kwa
halmashuri,fedha za mapato zitakazo saidia ujenzi wa miradi mbali mbali kwenye
jamii.
Kaimu Afsa Kilimo wa Wilaya ya
Tanganyika Yusuph Mukhandy amewaomba wakulima wote kuwa wanazingatia utaratibu
uliowekwa kwa ajili ya manufaa yao.
Vilevile kutokana na kuwa mfumo huo
kuwa mara ya kwanza kutamburishwa wakulima wanapaswa kuepuka kuuza mazao yao
kienyeji ambapo kwa kufanya hivyo hawataweza kunufaika na kilimo chao.
Comments
Post a Comment