Skip to main content

WALTEREED WATOA MSAADA WA VIFAA TIBA KATAVI KUPAMBANA NA COVID 19




 
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Comrade Juma Homera wa kwanza kutoka kulia akikabidhiwa box ya vifaa kutoka shirika la WalterReed na Dkt Shabain Ndama wa kwanza kutoka kushoto kwenye picha.



Na Mwandishi Wetu
       Katavi

Serikali ya Mkoa wa Katavi katika kuendelea kukabiliana na ugonjwa wa  COVID-19 imefanikiwa kupokea vifaa  tiba kutoka shirika la WalteReed vyenye thamani ya milioni ishirini na tano ili kuhakikisha mkoa huo haupatikani na mgonjwa hata mmoja wa virusi hivyo.

Mkoa huo hapo awali ulikabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba wa vitendea kazi kama vile Scaner kwenye baadhi  ya vituo vya vizuizi kwenye mipaka yake ya Burudi  na DRC Congo.
Akikabidhi vifaa hivyo Meneja Mradi WalterReed (HJFMRI) Mkoa wa  Katavi  Dkt Shabain Ndama mbele ya  Mkuu wa Mkoa huo Juma Homera  amesema kuwa vifaa hivyo vimetolewa ili kuendelea kuthibiti maambukizi  ya ugonjwa wa COVID 19.

Ndama alieleza kuwa vifaa hivyo vimetolewa kwa awamu ya kwanza  ni Scaner sita vya kisasa kwa ajili ya kupima joto la mwili,Madawa za kuuwa wadudu picks 300,Grovs pea 72 pamoja na Dawa za kuuliza maumivu ambavyo vimegharimu jumla ya milioni ishirini na tano. 

Pia wanatarajia  kuleta katika awamu ya pili  ni vitakasa mikono na barakaoa ambavyo vitasaidia watu kutumia ili kujikinga na maabukizi ya COVID 19.

Juma Homera Mkuu wa Mkoa wa Katavi akizungumza baada ya kupokea vifaa hivyo mbali na kuwa pongeza walterReed amewata walaamu wa afya kuhakikisha vifaa vinafika sehemu husika ili kukabiriana na Corona.

Mkuu wa mkoa huo ametoa wito kwa Madaktari kuendelea kutumia vifaa hivyo kwa uagalifu kwa sababu vifaa vilivyopobado ni vichache na kwa namna ambavyo wanaendelea kupokea vifaa kutoka kwa wadau mbalimbali vitasaidia mapambano hayo.

“katika maeneo ya mipaka hususani Mishamo wilaya ya Tanganyika hatukuwa na vifaa ambapo kuna wageni wengi kutoka nchi ya Burudi  wanao zunguka hadi Mkoa wa Kigoma na wengine wanaigilia ziwa Tanganyika kutoka nchi ya DRC Congo …pamoja na eneo la kata ya Kasakatengule huko kote hatukuwa na Scaner” Alisema Homera.

Pamoja na hayo Mkuu wa Mkoa huyo alisema kuwa hadi sasa katika mkoa wamefanikiwa kuweka watu wanne Karatini huku kukishuhudiwa kuwa hakuna mtu hata mmoja aliyepatikana  na maabukizi ya COVID 19.   

Magaga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Omary Sukari aliweka wazi kuwa kabla ya kupata vifaa hivyo kupatikana walikuwa wanakabiliwa na changamoto ya uhaba wa vifaa.

Hivyo Dkt Sukari alisema kuwa vifaa hivyo vitasaidia sana katika mapambono ya COVID 19 na kuwajengea uhakika wa kazi wanayoifanya kama madaktari ya kutokomeza virusi hivyo.

Comments

Popular posts from this blog

Tabasamu hili kwa Wanafunzi,Nuru imewaka Juu yao/Mwekezaji afanya Jambo ...

Ajira Mpya Wakaribishwa Mlele, Full Kula Bata/Makubwa yaja

Katavi Yakemea Vikali Ushoga,Mauaji "Wanaume Msiwazuie Wake Zenu Kufanya...