JESHI LA POLISI KATAVI LAPEWA MASAA 48 KUMPELEKA RAIA WA CHINA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA KUSHINDWA KUNAWA MIKONO
Na Mwandishi Wetu
Katavi.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma
Homera ametowa saa 48 kwa jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi kumfikisha Mahakamani
Raia wa Nchi ya China aitwaye Lin Guosong (34) mfabiashara Mkazi wa
Mtaa wa Majengo Manispaa ya Sumbawanga ambae alikamatwa kwa tuhuma za
kukataa kutii mashariti ya kujikinga na ugonjwa wa Corona COVID -19.
Homera alitowa maagizo hayo
hapo (leo) jana mbele ya wandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa
vifaa tiba vya kujikinga na ugonjwa wa COVID -19.
Vifaa hivyo vyenye thamani ya
zaidi ya shilingi Milioni 25 vilitolewa na shirika la Walter Reed walivyokabidhi
msaada kwa Mkuu wa Mkoa na Meneja wa mradi Walter Reed (HJFMRI) Dkt Shaban
Ndama .
Alisema Raia huyo wa Nchi ya
China alikamatwa na jeshi la polisi katika eneo la Kijiji cha
Kasansa Tarafa ya Mamba Wilayani Mlele Mkoani Katavi na kisha kupelekwa
katika kituo cha polisi cha Majimoto baada ya kukataa kutii amri ya kujikinga
na ugonjwa wa Corona kwa kukataa kunawa maji yenye dawa .
Alieleza kuwa raia huyo wa
nchi ya China alikamatwa katika Kijiji cha Kasansa Tarafa ya Mamba
Wilayani Mlele Mkoani hapa baada ya kukaidi agizo la kukinga na
kujiadhari na ugonjwa corona
.
Raia huyo wa china
siku hiyo akiwa kwenye kizuizi alitakiwa na kamati maalumu ya
Mkoa kuna maji yenye dawa kwa ajiri ya kujiadhari na kujikinga na maambukizi ya
corona .
Pamoja na kutakiwa kutekeleza
agizo hilo Raia huyo wa China Lin Guosong alikaidi hari ambayo
ilifanya polisi wa mkamate na kumfikisha katika kituo cha polisi cha maji
moto .
Alisema baada ya kuwa
amekamatwa yeye Mkuu wa Mkoa aliagiza mtuhumiwa huyo
hati yake ichukuliwe na iwe chini ya jeshi la polisi .
Mkuu wa Mkoa Homera aliagiza
kuwa kutokana na kitendo hicho cha Raia wa China kukaidi amri halali ya
Serikali ya Mkoa wa Katavi analiagiza jeshi la Polisi RPC Mkoa wa
katavi kuhakikisha ndani ya saa 48 wanamfikisha Mahakamani Raia huyo wa china
ili akajibu tuhuma zinazomkabili .
Alisisitiza kuwa Mkoa huu
umejipanga kuhakikisha wanajikinga na ugonjwa wa corona hivyo mtu yoyote ambae
atakaidi maagizo yaliyotolewa atachukuliwa hatua bila kujari cheo
cha mtu au rangi ya mtu .
Amewaonya watu wanao ishi
kwenye makazi ya wakimbizi ya Katumba na Mishamo waliokuwa raia ya nchi ya
Burundi ambao wamepewa uraia wa nchi ya Tanzania kuacha tabia ya kuwapokea
ndugu zao wanaotoka nchi ya Burundi kwa kuingia nchini kwa kupitia njia
ambazo sio rasmi kwani wanaweza kusababisha kuwepo kwa corona.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa
Katavi Dkt Omari Sukari alisema mpaka sasa Mkoa wa Katavi hauna
mgonjwa hata mmoja alipatikana na maambukizi hayo ila wanawashikilia watu wanne
waliowaweka kwenye karantini raia wa nchi ya DRC walioingia nchini kwa njia za
panya kwa kupitia mwambao wa ziwa Tanganyika.
Alisema Mkoa huu wamejipanga
kuhakikisha uonjwa huu hauingii kabisa katika Mkoa na kauli mbiu yao ya Mkoa ni
Mkoa wa Katavi bila Corona covid 19 inawezekana .
Comments
Post a Comment