Sehemu ya Wananchi wa Luhafwe wakiwa wamejitokeza kupata chanjo ya UVIKO-19 leo Oktoba 31,2022. Mratibu wa chanjo Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, Philip Mihayo. Zawadi Dakika,Afisa miradi kutoka Taasisi ya Benjamini Mkapa Shaban Juma,Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika. Dokta Alex Mrema,Mganga Mkuu Wilaya ya Tanganyika. Na Aidan Felson,Site Blog-Katavi. ****************************************** HALMASHAURI ya Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi kwa kushirikiana na Taasisi ya Benjamini Mkapa imefanikiwa ndani ya siku Saba kuwafikia na kuchanja Watu 32,000 wa chanjo ya kuzuia ugonjwa wa UVIKO-19 katika Halmashauri hiyo, kupitia kampeni ya uhamasishaji wa uchanjanji nyumba kwa nyumba ya siku Tisa. Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la Kijiji cha Luhafwe sehemu iliyotengwa maalum kwa ajili ya utoaji chanjo,Mratibu wa chanjo Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, Philip Mihayo amesema idadi hiyo imefikiwa kutokana na hamasa na mbinu shirikishi iliyotumika...