Skip to main content

MKOA WA KATAVI KUZALISHA TANI MILIONI 1.2 ZA CHAKULA 2022/23.




Picha ikiwaonyesha Wakurugenzi watendaji,wa Kwanza Kulia ni Bi. Catherine Mashala (Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mpimbwe),wa Pili ni Mohamed Ramadhan (Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nsimbo),wa Tatu ni Theresia Irafay (Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mlele) na wa mwisho ni Sophia Kumbuli (Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda).


Wakuu wa Wilaya,kushoto ni Onesmo Buswelu (Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika) na Filberto Sanga (Mkuu wa Wilaya ya Mlele) wakifurahia jambo.

Jamila Yusuf,Mkuu wa Wilaya ya Mpanda akizungumza kwa niaba ya Wakuu wa Wilaya wenzake katika kilele cha wiki ya mwana Katavi na uzinduzi wa msimu mpya wa Kilimo 2022/22.

Mwanamvua Mrindoko,Mkuu wa Mkoa wa Katavi akizungumza katika kilele cha wiki ya mwana Katavi na uzinduzi wa msimu mpya wa Kilimo 2022/22.


Na Aidan Felson,Site Blog-Katavi.
********************************************

MKOA wa Katavi Jana Nomba 2,2022 umezindua msimu mpya wa Kilimo 2022/23,uzinduzi uliofanyika katika viwanja vya Shule ya msingi Kashato Manispaa ya Mpanda wakati wa kuhitimisha kilele cha wiki ya mwana Katavi iliyoanza Oktoba 28,2022.

Akifunga wiki hiyo na kufungua msimu mpya wa kilimo,Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amesema katika msimu mpya wa Kilimo 2022/23 Mkoa wa Katavi una malengo ya kulima Hekta 339,187 zikiwemo Hekta 273,436 za mazao ya chakula na Hekta 65,752 za mazao ya Biashara.

RC Mrindoko amesema katika msimu wa kilimo 2022/23 Mkoa wa Katavi una lengo la kuzalisha Tani 1,159,754 ikiwemo Tani 1,074,187 za mazao ya chakula na Tani 85,568 za mazao ya Biashara.

Katika kuhakikisha Mkoa unazalisha kiasi hicho cha mazao, RC Mrindoko amesema Mkoa unahitaji Tani 14,811 za mbolea.

Aidha,kutokana na dhamira ya Serikali ya awamu ya Sita kuhakikisha inawainua wakulima, Mrindoko ametoa wito kwa wakulima wote Mkoani humo kujitokeza na kujiandisha katika daftari la wanufaika wa mbolea za ruzuku kwani kila mkukima atapata mbolea kulingana na mahitaji yake ili kumwezesha kuzalisha kwa tija.

Ili kufikia malengo hayo, Mrindoko amewataka wakulima kuwa waaminifu kwa kufanya matumizi ya mbolea kama ilivyo kusudiwa na sio kwenda kuiuza ambapo ili kudhibiti hilo amewaagiza wakuu wa wilaya kuhakikisha wanafuatilia kila Mkulima ili kujua kama matumizi ya mbolea yanakwenda sambamba na lengo la Serikali.

"Niwaombe wakulima,tumieni hii fursa vizuri. Serikali ya Mama Samia Suluhu Hassan imewaletea mbolea ya ruzuku,itumieni vizuri kwa kuwa waaminifu kwa kuchukua mbolea na kwenda kuitumia kwenye shamba lako ili ukaongeze tija"-Amesema Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,wakati akikagua banda la wauzaji mbolea aina ya Yara.

Kadhalika,amesema Mkoa wa Katavi katika msimu wa mwaka wa kilimo 2020/21 uliweza kuvuna Tani 1,173 za Pamba na kwa msimu wa 2021/22 Mkoa uliweza kuzalisha Tani 5,340.

"Hongereni Bodi ya Pamba,Hongereni NGS,hongerini sana wakulima wetu kwa kufuata maelekezo ya bodi ya Pamba...tunapokwenda kuanza msimu mpya wa kilimo,hakikisheni mnaongeza mshamba lakini kwa kuzingatia maelekezo ya wataalamu"

Licha ya kusisitiza wananchi kuwekeza katika kilimo, Mkuu huyo wa Mkoa ametoa wito kwa wananchi kujiwekea akiba ya chakula badala ya kuuza chote kwa kuwa msimu huu kuna uwezekano mvua zikawa chache.

"Huko nje kwenye Mikoa mingine na Nchi nyingine HALI SIO NJEMA,kuna njaa ya hali ya juu. Naomba sana niwaombe tena na tena wananchi wa Mkoa wa Katavi,kila familia,kila kaya hifadhi chakula cha kulutosha wewe kulingana na idadi ya wana kaya ulionao"

Katika sekta ya utalii,RC Mrindoko ameagiza vivutio vyote vilivyopo ndani ya Mkoa huo vinatangazwa ili kuvutia watalii wengi ikiwemo kuwafikia Wananchi wa Mkoa huo kwa njia mbalimbali kuhusu vivutio vyilivyopo Mkoani humo.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko alipopita banda la maonesho la Maliasili na Utalii na kutoa maelekezo akizitaka sekta ya maliasili kusimamia utunzaji misitu na sekta ya utalii kutangaza vivutio vilivyopo Mkoani humo.

Vile vile amezionya Taasisi ambazo hazijashiriki maadhimisho hayo huku akiagiza Halmashauri zote na Taasisi zote za Umma Mkoani humo kuhakikisha mwakani zinashiriki wiki ya mwana Katavi kwa asilimia Mia moja bila kisingizio cha aina yoyote.

Kwa upande wao baadhi ya Wananchi wa Manispaa ya Mpanda wakizungumza na chanzo hiki eneo la Viwanja vya maonesho wamesema watazingatia ushauri wa Mkuu wa Mkoa kwa hukahikisha wanabakiza akiba ya chakula.

"Tuache tamaa kwa sababu ukiuza utalazimika kurudi sokoni kununua tena...nawashauri wale Wazazi wanaouza mazao kwa ajili ya kwenda kunywa pombe waache"-Alissma Magdalena Simon.

Kwa upande wao wadau walioshiriki Wiki ya mwana Katavi wamepongeza hatua za Serikali Mkoani humo kuandaa maonesho hayo kwani kwao yamekuwa na tija kubwa.

Naye Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf akizungumza kwa niaba ya wakuu wenzake wa wilaya amemhakikishishia Mkuu wa Mkoa kuwa yeye na wenzake watakwenda kusimamia maelekezo yote aliyoyatoa.

"Tunakushuruku moja ya maelekezo ambayo umeyatoa umesema hii wiki ya mwana Katavi itakuwa inafanyika kila mwaka, tunakushuruku sana mkuu wa Mkoa kwa hilo"

Mkoa wa Katavi umeanzisha wiki ya mwana Katavi yenye lengo la kuwapa fursa wakulima na wajasiriamali kuonyesha bidhaa zao huku lengo kuu likiwa ni kutoa elimu kwa wakulima juu ya mauala mbalimbali yahusuyo kilimo.

Maonyesho hayo ya ndani ya Mkoa yameanza mwaka huu ambapo yalianza Oktoba 20,2022 kwa kufanyika shughuli mbalimbali zikiwemo maonyesho ya kilimo,utalii wa ndani kwa kutembelea vivutio katika hifhadhi ya Katavi sanjari na shindano la Miss Utalii Katavi 2022.


Picha ikiwaonyesha ma Miss Utalii Katavi 2022.

Kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi ya Mwaka 2022,Mkoa wa Katavi una jumla ya watu 1,152,958 kutoka Watu 564,604 kwa sensa ya Mwaka 2012 huku Idadi hiyo ikitajwa kuwa huenda ikaongeza kasi ya uzalishaji wa chakula endapo Wananchi wataamua kuwekeza kwenye kilimo na uzalishaji mwingine.

MWISHO.

Comments

Popular posts from this blog

WAJASIRIAMALI MPANDA WAILILIA SERIKALI KUCHELEWA UPATIKANAJI WA VITAMBULISHO

Na Swaumu Katambo, Katavi W afanyabiashara wadogo   katika stendi ya mabasi M izengo P inda wameiomba S erikali kuharakisha ugawaji wa vitambulisho ili kuep u kana na adha ya kulipa ushuru wa H almashauri ambao una   gharama  kubwa. W akizungumza na Site Tv  wajasiriamali M jini M panda wame i lalamikia H almashauri ya M anispaa ya M panda kuwatoza ushuru pasipo kuwa na utaratibu wowote . Mkurugenzi wa M anispaa ya M panda M ichael N zyungu amesema kuwa adha hiyo imetokana na kuchele we shwa kwa vitambulisho na amewataka wajasiriamali kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki. Vitambulisho vya ujasiriamali vilianzishwa na serikali maalumu kwa kuwasaidia wafanya   biashara wadogo kutoa huduma bila bugdha yoyote . MWISHO

Tufanye mabadiliko ya kina kwenye mfumo wa elimu -Mbunge Rose Tweve

KANISA KATOLIKI PAROKIA YA INYONGA LAFANYA MISA MAALUMU KUMUOMBEA DKT MAGUFULI, DC JAMILA ASISITIZA KUMUENZI KWA VITENDO

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda  ambaye pia ni  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mlele  Mhe  Jamila Yusu ph akisisitiza jambo wakati  akizungumza kwenye Misa Maalumu katika Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Mkuu wa Wilaya ya Mpanda  ambaye pia ni  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mlele  Mhe  Jamila Yusu ph akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Kanisa katoliki Parokia ya inyonga mara baada ya kumalizika  Misa Maalumu ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Kiongozi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga Padri  Maricelo Butoyi akiongoza Misa Maalumu ya  kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Sehemu ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga wakifuatilia ibada Maalumu ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Sehemu ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga wakifuatilia ibada Maalumu ...