Skip to main content

MALEZI YA WATOTO YAGUBIKA KONGAMANO LA WANAWAKE - MPANDA.

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf akizungumza jambo katika kongamano la kuelekea siku ya wanawake Duniani Machi 8, lililofanyika katika Ukumbi wa Mpanda Municipal Social Hall Mjini Mpanda alipomwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mwanamvua Mrindoko.



Baadhi ya Wanawake walioshiriki Kongamano la kuelekea siku ya Wanawake Duniani lililofanyika Mjini Mpanda leo Machi 7,2022.

                  ***************************************

                              Na.Swaum Katambo

                                 Mpanda-Katavi

Wanawake Mkoani Katavi wametakiwa kusimama imara katika eneo la malezi ili kuepusha makundi mbalimbali ya kihalifu yanayojiita Damu chafu, Manyigu, Mapopo, Kabuli wazi na mengineyo yanayoongozwa na watoto yenye kuhatarisha hali ya usalama wa wananchi.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf alipomwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Katavi katika Kongamano la kuelekea siku ya wanawake Duniani lililofanyika Mjini Mpanda ambapo amesema kuwa wanawake ndio chachu ya matukio ya kihalifu ya watoto wao kwakuwa wanapokamatwa na vyombo vya usalama huwatetea.

"Wakinamama tumekuwa tukiwatetea sana, mtoto wako akikamatwa unasema aah jamani hata nilikuwa sijui kabisa kama anashiriki hivi vitendo, na mara nyingine wamediriki hata kuniomba mie niwatoe wakikamatwa huko, 'naomba uwatoe mama', yaani wanatetea ujinga" , Aliongea kwa uchungu DC Jamila

"Hao watoto tumewazaa sisi,wamezaliwa na mtu anayeitwa mwanamke hivyo waliochangia uwepo wa kizazi hiki haribifu ni sisi wanawake.., tuwalee watoto wetu kimaadili,Kiroho na kimwili ili kuepusha makundi haya yanayohatarisha usalama wetu"

DC Jamila ametolea mfano wa Kata ya Shanwe iliyopo Mjini Mpanda kuwa na hali mbaya kiasi ambacho walimu wa shule wanatamani kukimbia huku akiongeza kuwa wanaowatesa walimu hao ni wanafunzi ambao wamekataa kwenda shule.

Hata hivyo ameongeza kuwa vyombo vya sheria vinavyolinda haki za watoto viangalie vizuri sheria zao ili kudhibiti matukio hayo kwani pindi vyombo vya dola vinapotekeleza majukumu ya kuzuia matukio ya kihalifu ya watoto hukutana na kizingiti cha kulinda haki za watoto.

"Wakinamama wa Mkoa wa Katavi hasa wa Wilaya ya Mpanda tusimame vizuri tuwadhibiti watoto wetu,hata kama mtoto si wako ukimchekea ipo siku atakudhuru, na Mkishindwa kuwadhibiti basi tutawasaidia". Aliongeza

Hata hivyo amewataka pia wakinamama kuhakikisha wanakaa na kuzungumza na watoto wao wakike ili kuwalinda dhidi ya ukatili wa kijinsia huku akisema kuwa wanaoendeleza ukatili huo ni wanawake.

"Mtoto amechaguliwa kidato cha kwanza unaenda kumuozesha unataka ng'ombe,ni vizuri kuweka utaratibu wa kuongea na watoto wetu na kuwaweka wazi ni vitu gani wakifanyiwa ni ukatili,ukatili si hadi mtoto abakwe au alawitiwe", Alisema DC Jamila

Kwa upande wao baadhi ya kinamama wamekiri kuchangia kwa kiasi kikubwa kushindwa kulea watoto wao vizuri kwani wengine wamekuwa wakiwatuma watoto kwenda kutafuta pesa kwa ajili ya chakula na huku wengine wanapoambiwa na majirani zao mienendo ya watoto wao huwatetea.

"Kuna wazazi wanatuma watoto kwenda mitaani kutafuta chochote kile kwa ajili ya chakula kwahiyo wanapokamatwa yeye anaona heri amtetee mtoto wake na kuhisi mtoto wake ameonewa"Alisema Magreth Alex mkazi wa Kata ya Makanyagio

"Sisi tunajidai tuna uchungu Sana kuliko kina baba,tukifikiria ule uchungu jinsi ya kumzaa basi unaona ukimtetea ndio unaona unamjali kumbe unamharibu", Alisema Mama Babu Mkazi wa Kata ya Majengo 'A'

Hivi karibuni kumekuwa na matukio mbalimbali ya kihalifu yanayofanywa na vikundi vya watoto wanaozurula mtaani na kusababisha madhara katika jamii yakiwemo kupora,kuiba na kujeruhi na kufanya wakazi mjini Mpanda kujawa na hofu ya kutembea majira ya usiku wakiogopa kukutana na watoto hao.

MWISHO

Comments

Popular posts from this blog

WAJASIRIAMALI MPANDA WAILILIA SERIKALI KUCHELEWA UPATIKANAJI WA VITAMBULISHO

Na Swaumu Katambo, Katavi W afanyabiashara wadogo   katika stendi ya mabasi M izengo P inda wameiomba S erikali kuharakisha ugawaji wa vitambulisho ili kuep u kana na adha ya kulipa ushuru wa H almashauri ambao una   gharama  kubwa. W akizungumza na Site Tv  wajasiriamali M jini M panda wame i lalamikia H almashauri ya M anispaa ya M panda kuwatoza ushuru pasipo kuwa na utaratibu wowote . Mkurugenzi wa M anispaa ya M panda M ichael N zyungu amesema kuwa adha hiyo imetokana na kuchele we shwa kwa vitambulisho na amewataka wajasiriamali kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki. Vitambulisho vya ujasiriamali vilianzishwa na serikali maalumu kwa kuwasaidia wafanya   biashara wadogo kutoa huduma bila bugdha yoyote . MWISHO

Tufanye mabadiliko ya kina kwenye mfumo wa elimu -Mbunge Rose Tweve

KANISA KATOLIKI PAROKIA YA INYONGA LAFANYA MISA MAALUMU KUMUOMBEA DKT MAGUFULI, DC JAMILA ASISITIZA KUMUENZI KWA VITENDO

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda  ambaye pia ni  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mlele  Mhe  Jamila Yusu ph akisisitiza jambo wakati  akizungumza kwenye Misa Maalumu katika Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Mkuu wa Wilaya ya Mpanda  ambaye pia ni  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mlele  Mhe  Jamila Yusu ph akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Kanisa katoliki Parokia ya inyonga mara baada ya kumalizika  Misa Maalumu ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Kiongozi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga Padri  Maricelo Butoyi akiongoza Misa Maalumu ya  kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Sehemu ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga wakifuatilia ibada Maalumu ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Sehemu ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga wakifuatilia ibada Maalumu ...