Skip to main content

LIGI KUU KUNA MAMBO YA HOVYO YANAENDELEA, TFF CHUKUENI HATUA-WAZIRI BASHUNGWA.



Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa akizungumza jambo katika Mashindano ya Michezo na Sanaa Vyuo vya Ualimu yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Mtwara.



Mashindano yakiendelea huku Mashabiki wakifatilia.






                    *****************************************************
                                Na,Mwandishi Wetu.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amelitaka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF kuwachukulia hatua waamuzi wa mpira wanao onekana kufanya mambo ya hovyo katika ligi kuu ya Tanzania inayoendelea.

Waziri Bashungwa ametoa agizo hilo jana Desemba 05, 2021, wakati akiongea na waandishi wa habari mkoani Mtwara katika kilele cha mashindano ya kitaifa ya Michezo na Sanaa ya vyuo vya ualimu UMISAVUTA yaliyofanyika mkoani humo  kuanzia Novemba 29, 2021.

Waziri Bashungwa amesema licha ya ligi Kuu ya Tanzania kuendelea vizuri lakini kumekuwepo na waamuzi wanaofanya mambo ya hovyo ambayo siyo tu yanashusha adhi yao lakini yanavunja imani, amani na mioyoo ya wachezaji na mashabiki wa timu zinazofanyiwa mambo hayo.

“We fikilia kuna klabu unakuta inachangishana shilingi elfu 10, au elfu tano ili hiyo klabu ikacheze sehemu fulani, inatoka Mkoa A inaenda Mkoa B alfu mwamuzi anafanya mambo ya uonevu uwanjani, hilo jambo linamuumiza si tu klabu ile ila hata yule aliyechangia elfu tano yake ili timu yake ikacheze” alisema Waziri Bashungwa.

Aliongeza kuwa “Kwahiyo inapotokea Waamuzi wachache wanataka kudhoofisha michezo kwakweli tusiwafumbie macho, Kwahiyo wito wangu kwa TFF wasipepeshe macho, wawe wakali, watumie sheria na  kanuni zilizopo kuhakikisha waamuzi ambao wanafanya mambo ya hovyo kwenye viwanja, wawachukulie hatua  ili tusivikatishe tama vilabu vinavyoangaika sana kupata rasilimali fedha.

Akizungumzia mashindano hayo ya UMISAVUTA Waziri Bashungwa amesema Wizara yake itaendelea kushirikiana kwa karibu na Wizara ya Elimu pamoja na Ofisi ya Rais TAMISEMI kuhakikisha mahitaji ya walimu wa michezo shuleni yanaendana na uzalishaji wa walimu hao kwenye vyuo wa ualimu.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo amesema dhamira ya kurejeshwa kwa mashindano hayo ambayo yalikuwa yamesitishwa kwa zaidi ya miaka 20 iliyopita, ni kuwatengeneza walimu wanafunzi, kuwa imara katika michezo wenye ujuzi na uwezo wa kushiriki na kuendesha michezo katika shule watakazopangiwa pindi wanapo hitimu masomo yao.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Mashindano hayo kwa mwaka 2021 Doroth Mhaiki amesema matarajio yao ni kuona vyuo vya ualimu Tanzania vikishiriki katika mashindano mbalimbali ya Afrika Mashariki.

Mashindano hayo ya UMISAVUTA yameusisha Michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mpira, riadha, fani za ndani na mashindano ya ubunifu wa vifaa vya kufundishia ambapo kanda ya Mashariki imeibuka bingwa katika mchezo wa soka huku Kanda ya Ziwa ikiibuka mshindi wa jumla kwa kubeba vikombe vingi zaidi katika mashindano hayo.

MWISHO.

Comments

Popular posts from this blog

WAJASIRIAMALI MPANDA WAILILIA SERIKALI KUCHELEWA UPATIKANAJI WA VITAMBULISHO

Na Swaumu Katambo, Katavi W afanyabiashara wadogo   katika stendi ya mabasi M izengo P inda wameiomba S erikali kuharakisha ugawaji wa vitambulisho ili kuep u kana na adha ya kulipa ushuru wa H almashauri ambao una   gharama  kubwa. W akizungumza na Site Tv  wajasiriamali M jini M panda wame i lalamikia H almashauri ya M anispaa ya M panda kuwatoza ushuru pasipo kuwa na utaratibu wowote . Mkurugenzi wa M anispaa ya M panda M ichael N zyungu amesema kuwa adha hiyo imetokana na kuchele we shwa kwa vitambulisho na amewataka wajasiriamali kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki. Vitambulisho vya ujasiriamali vilianzishwa na serikali maalumu kwa kuwasaidia wafanya   biashara wadogo kutoa huduma bila bugdha yoyote . MWISHO

Tufanye mabadiliko ya kina kwenye mfumo wa elimu -Mbunge Rose Tweve

KANISA KATOLIKI PAROKIA YA INYONGA LAFANYA MISA MAALUMU KUMUOMBEA DKT MAGUFULI, DC JAMILA ASISITIZA KUMUENZI KWA VITENDO

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda  ambaye pia ni  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mlele  Mhe  Jamila Yusu ph akisisitiza jambo wakati  akizungumza kwenye Misa Maalumu katika Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Mkuu wa Wilaya ya Mpanda  ambaye pia ni  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mlele  Mhe  Jamila Yusu ph akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Kanisa katoliki Parokia ya inyonga mara baada ya kumalizika  Misa Maalumu ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Kiongozi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga Padri  Maricelo Butoyi akiongoza Misa Maalumu ya  kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Sehemu ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga wakifuatilia ibada Maalumu ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Sehemu ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga wakifuatilia ibada Maalumu ...