Picha na Mtandao.
**********************************************
Na Irene Temu,Katavi.
Ukosefu wa uhamasishaji kwa umma kuhusu huduma za lishe zinazopatikana kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano na Mama wajawazito ndio tatizo kubwa la kuendelea kuwa na utapiamlo.
Ambapo ukosefu wa lishe mchanganyiko na bora kwa kila kaya kutokana na kipato kidogo katika familia huchangia huku Elimu juu ya lishe ikihitajika.
Akizungumza na Mwandisi wa Habari hizi Afisa lishe Mkoa wa Katavi Asnath Mrema alisema kuwa Mwili kupokea virutubishi vya lazima Kama kalori,protini,mafuta,wanga, vitamini na madini uhaba au wingi wa vitu hivyo katika mwili husababisha utapiamlo.
Sambamba na kukosa chakula cha kutosha na mtoto kukaa na njaa ya muda mrefu au kushiba bila kujali uwiano wa virutubishi ndani ya chakula nayo Ni sababu mojawapo ya mtoto kupata utapiamlo
Aidha aliongeza kuwa udumavu huweza kutokea kati ya siku moja tangu kutungwa mimba Hadi siku 1000 hivyo mama mjamzito anatakiwa kupata lishe Bora Ili kuweza kurutubisha Afya ya Mwili wake na kiumbe aliyeko tumboni.
Pia alisema kuwa kupitia Mpango wa Utekelezaji wa lishe ya kitaifa wa Mwaka 2016-2021 Asilimia 31.5 ya Watoto chini ya Miaka Mitano wanaudumavu kutoka Asilimia 88 ya Mwaka 1999.
Hivyo aliitaka jamii kuboresha namna ya ulishaji wa Watoto wachanga na wadogo na kushauri pia kunyonyesha kunapunguza viwango vya utapiamlo na vifo kwa watoto.
Nae Daktari Erick Mwijage aliongeza kuwa maradhi ya kuambukiza kama homa ya matumbo,nimonia,malaria huongeza mahitaji ya lishe hivyo endapo mtoto atakosa huishia kupata utapiamlo.
"Endapo ukosefu wa lishe utatokea wakati wa ujauzito au kabla ya umri wa miaka miwili huenda ukasababisha matatizo ya kudumu katika ukuaji wa Mwili,akili,kimo cha chini,wembamba,viwango vya chini sana vya nguvu, miguu pamoja na tumbo kuvimba"alisema Daktari Erick
Pia alisema kuwa zipo aina mbili za ukosefu wa lishe ambapo alifafanua kwamba kuna ukosefu wa Lishe ya Protini ambayo huleta nguvu Mwilini na kusababisha Mtoto kuwa na unyafuzi.
Huku ukosefu wa lishe Bora ni Mtoto kukosa vyakula vyenye aina zote za virutubisho na Madini kama Ayodini na Vitamin A.
Hivyo jamii imetakiwa kizingatia chakula cha nyongeza kwa Watoto kati ya miezi 6 na miaka miwili huku kilimo kikiboreshwa kwa ajili ya kupata chakula cha kutosha Ili kupunguza umasikini na kuondoa uchafu katika mazingira yanayotuzunguka ili kupunguza magonjwa.
Sambamba na kuwawezesha wanawake kiuchumi kwani ndio nguzo kubwa katika kulea familia pamoja na Watoto.
MWISHO.
Comments
Post a Comment