Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akionesha andiko kwa Wafanyabiashara wa Mazao ya Misitu katika Mkutano la Kiwanda cha Edosama Hadware Ltd kinachomilikiwa na Mtanzania, Edward Maduhu ambacho kimekuwa kikitengeneza bidhaa mbalimbali hapa hapa nchini hadi hatua za mwisho kwa kutumia vinia, Kulia ni Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa, Mkutano huo umefanyika Jijini Dar es Salaam. Baadhi ya Wafanyabaishara wa mazao ya misitu nchini wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro katika mkutano uliofanyika Jijini Dar es Salaam ambapo amewataka Wafanyabishara hao kuleta mashine za kuchakata vinia hadi hatua za mwisho ili kutoa ajiara kwa wananchi wanaozunguka misitu nchini. Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza katika mkutano wa Wafanyabiashara wa Mazao ya Misitu ambapo ametoa ruhusa ya kusafirisha vinia kuanzia leo hadi tarehe 30 Juni 2022 kwa vigezo...