Skip to main content

WAZIRI NDUMBARO ATOA RUHUSA YA KUSAFIRISHA MAKONTENA 187 YA VINIA KWENDA NCHI ZA NJE.



Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akionesha andiko kwa Wafanyabiashara wa Mazao ya Misitu katika Mkutano  la  Kiwanda cha Edosama Hadware Ltd kinachomilikiwa na  Mtanzania, Edward Maduhu ambacho kimekuwa  kikitengeneza bidhaa mbalimbali hapa hapa nchini hadi hatua za mwisho kwa kutumia vinia, Kulia ni Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa, Mkutano huo umefanyika Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Wafanyabaishara wa mazao ya misitu nchini wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro  katika mkutano uliofanyika Jijini Dar es Salaam ambapo amewataka Wafanyabishara hao kuleta mashine za kuchakata vinia hadi hatua za mwisho ili kutoa ajiara kwa wananchi wanaozunguka misitu nchini.


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza katika mkutano wa Wafanyabiashara wa Mazao ya Misitu ambapo ametoa ruhusa ya kusafirisha vinia kuanzia leo hadi tarehe 30 Juni 2022 kwa vigezo na masharti kuzingatiwa.


                   - Atoa kipindi cha mpito cha kusafirisha vinia hadi hadi tarehe 30  Juni 2022

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro ameruhusu kusafirisha makontena 187 ya Vinia kwenda nchi za nje  yaliyokuwa yamekwama  bandarini baada ya kutoa tamko la  kuzuia usafirshaji malighafi za mazao ya misitu kwenda nchi za nje  ikiwemo vinia

Vinia ni malighafi iliyochakatwa nusu kutoka kwenye gogo ambalo Wawekezaji wengi husafirisha nje ya nchi kwa ajili ya kutengeneza bidhaa mbalimbali  hususan mbao laini (plywood) ambazo hurejeshwa tena nchini kuuzwa kwa bei ya juu

Plywood ndiyo inayotumika katika shughuli za ujenzi  wa maghorofa na kutenganisha vyumba katika ofisi, Licha ya kuruhusu usafirishaji wa  makontena hayo 187 yaliyokuwa na vinia, Dkt. Ndumbaro ameendelea kushikilia msimamo wake wa kutoruhusu uvunaji na biashara ya gundi ndani na nje ya nchi mpaka pale watafiti watakapotoa hasara na faida yake.

Hatua hiyo inakuja kufuatia ombi la Wafanyabishara wa mazao ya misitu wakimtaka  aongeze muda wa kusafirisha mazao ya misitu kwenda nchi za nje baada ya  kupigwa  marufuku kuanzia Novemba 15 mwaka huu.akiwa mkoani Iringa

Waziri Dkt. Ndumbaro ametoa ruhusa hiyo leo wakati alipokuwa akizungumza na k Wafanyabishara wa mazao ya misitu katika mkutano ulioitishwa na Wafanyabiashara hao Jijini Dar es Salaam kupitia Baraza la Taifa la Wafanyabishara (TNBC) wakiomba kuongezewa muda wa kusafirisha mazao hayo. 

Akifafanua ruhusa hiyo, Dkt. Ndumbaro amesema ruhusa hiyo  inahusu makontena 187  tu ambayo yapo tayari yameshafika  bandarini na sio kwa makontena ambayo hayako bandarini

''Naomba nieleweke vizuri ruhusa hii ya kusafirisha vinia itahusu makotena 187 tu ambayo nyaraka zake tayari zilishawasilishwa kwenye vyombo vya kiserikali'' amesisitiza Dkt, Ndumbaro

Katika hatua nyingine, Serikali imewaongezea muda Wafanyabiashara wa mazao ya misitu nchini kusafirisha vinia kuanzia leo hadi tarehe 30 Juni 2022 kwa  vigezo na masharti kuzingatiwa

Akitaja masharti hayo Dkt. Ndumbaro amesema  Wafanyabiashara  watakaoruhusiwa kusafirisha vinia kwa kwa kipindi hicho tajwa watatakiwa kuwasilisha mpango kazi  wa kuleta mashine ya kuchakata vinia hadi hatua za mwisho pamoja na kuwasilisha taarifa za kodi na malipo mengine ya serikali

Mbali na Mashart hayo, Dkt. Ndumbaro  amesema wafanyabiashara hao ili waweze kuruhusiwa kusafirisha mazao hayo watatakiwa kuwasilisha  taarifa za haki za Wafanyakazi katika viwanda vyao pamoja na gharama halisi za mzigo huo

Hata hivyo, Dkt. Ndumbaro ametoa onyo kwa Mfanyabishara yeyote atakayetoa taarifa za uongo na akathibitika hatapewa ruhusa ya kusafirisha vinia hiyo huku akisisitiza kuwa katika kipindi hicho cha mpito yeye mwenyewe Waziri ndiye aatakayehusika na kutoka vibali kwa Wafanyabishara vya kuruhusu kusafirisha vinia kwenda nchi za nje 

Kwa upande wake  Mwenyekiti Mwenza wa Baraza la Taifa la Wafanyabaishara (TNBC) Ben Sulus amemshukuru Waziri kwa kukubali ombi la Wafanyabishara hao la kuongezewa muda huku akisisitiza kuwa ni muda muafaka sasa kwa Wafanyabishara hao kuungana kwa pamoja kuleta mashine ambazo zitachakata vinia hozo hadi hatua za mwisho ili kutoa ajira kwa wananchi wanaozunguka misitu hiyo.

Naye Mfanyabishara wa Kiwanda cha Vinia cha Yu lin,Ben Makombe amesema  Wizara ina lengo jema lakini wanaomba kuongezwa muda takriban mika mitatu ili waweze kukusanya  fedha kwa ajili ya kununua mashine ambazo zitaweza kuchakata vinia hizo hadi hatua za mwisho

Amefafanu kuwa mashine hizo zinauzwa dola 8,000 hivyo zinahitaji Wafanyabaishara wenye mitaji mikubwa hivyo endapo watapewa muda wataweza kuzinunua.

MWISHO.

Comments

Popular posts from this blog

Mkuu wa Mkoa wa Katavi akibidhiwa Ofisi,aelezwa Miradi ya kusimamia.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi,Mwanamvua Hoza Mrindoko wa kwanza Kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera wakati wa makabidhiano ya Ofisi. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi Beda Katani. Wakuu wa Wilaya,Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Rachel Kasanda. Na Mwandishi Wetu,Site Tv Mapema leo Mei 25,2021 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko,amekabidhiwa Ofisi na aliye kuwa Mkuu wa Mkoa huo Juma Zuberi Homera aliye hamishiwa Mkoani Mbeya kuwa Mkuu wa Mkoa. Katika makabidhiano hayo,Homera amemtajia Mkuu wa Mkoa wa Katavi miradi ambayo inatakiwa kusimamiwa hadi ikamilike ni pamoja na Bandari ya Karema,Hosipitali ya Rufaa Mkoa,Kiwanda cha Nguo,Jengo la Utawala pamoja na Umeme wa Gridi ya Taifa. Aidha,amesema Katavi ni Nyumbani hivyo atatoa ushirikiano kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi huku akiwakaribisha Viongozi na Wananchi kwa ujumla katika Mkoa wa Mbeya. "Kuna hili la Gridi ya Taifa ambalo linaendelea,kuna Kiwan...

Tabasamu hili kwa Wanafunzi,Nuru imewaka Juu yao/Mwekezaji afanya Jambo ...

Ajira Mpya Wakaribishwa Mlele, Full Kula Bata/Makubwa yaja