Ikiwa Ujumbe Mkuu wa mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa kwa mwaka huu 2021 unasema "Tehama ni Msingi wa Taifa endelevu itumie kwa usahihi na uwajibikaji",Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Luteni Josephine Mwambashi leo Sep 24 amezindua Shughuli za TEHAMA katika Shule ya Wasichana Mpanda iliyopo Mkoani Katavi.
Baadhi ya wanafunzi Shule ya Wasichana Mpanda.Mwenge wa Uhuru pia umeweza kuzindua baadhi ya klabu mashuleni zikiwemo klabu ya Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI katika shule ya Msingi Uruwila,Klabu ya Mapambano dhidi ya Rushwa Shule ya Sekondari Nsimbo,Klabu ya mapambano dhidi ya dawa za kulevya Shule ya Msingi Kashato na Klabu ya lishe wanafunzi wa Shule ya Msingi Katavi.
Hata hivyo mwenge wa Uhuru umeweka mawe ya Msingi katika Miradi miwili ambayo ni Kituo cha Mafuta (MSS) na Ujenzi wa Barabara ya Mkumbo mita 600 kwa kiwango cha Lami.
Kadhalika, Mwenge wa Uhuru umezindua vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja shule ya Msingi Uruwila,Zahanati ya Shanwe huku Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Luteni Mwambashi akimalizia kwa kugawa vyandarua kwa mama wajawazito katika Zahanati hiyo.
Miradi yote iliyozinduliwa na kuwekwa mawe ya Msingi imeonekana kufanya vizuri ukilinganisha na gharama zilizotumika, isipokuwa Mradi mmoja wa Tanki la kuhifadhia Maji Ikolongo namba mbili uliopo eneo la Mapinduzi Kata ya Ilembo ambao umegharimu Tsh.Bil 1.7 Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru amekataa kuuzindua kwa kile alichodai gharama za ujenzi kuwa kubwa ukilinganisha na mradi huo.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Luteni Josephine Mwambashi.Hata hivyo kufuatia changamoto hiyo ya kukataliwa kwa Mradi wa Maji Ikolongo namba mbili,Mbunge wa Mpanda Mjini Sebastian Kapufi amewataka watumishi wanapopewa dhamana ya kusimamia Miradi kuwa waangalifu na kutofanya ubadhilifu wa mali yoyote ya umma.
Comments
Post a Comment