Skip to main content

MKOA WA KATAVI KUANZISHA HUDUMA MKOBA YA CHANJO.


Picha ya Kwanza ni Mwandishi wa Habari wa TBC Mkoani Katavi Bw.Hoseya Cheyo na ya Pili ni Mwandishi wa Habari kutoka Kituo cha Redio Pamoja Fm Mkoani Katavi Bw.Paul Mathias wakipata Chanjo kwa hiari ya UVIKO-19 baada ya kupata Elimu ya kutosha kuhusu Chanjo hiyo.


Picha ni baadhi ya Waandishi wa Habari Mkoani Katavi wakiwa na Wataalamu (Waliovaa nguo Nyeusi) wakielekezwa jambo.


Mkuu wa Mkoa wa Katavi akizungumza na Waandishi wa Habari Mkoani humo Ofisini kwake kuhusu mkakati wa kuanza huduma Mkoba ya Chanjo ya UVIKO-19.


Mwakilishi kutoka Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) Boniface Makelemo akizungumza jambo kwa Waandishi wa Habari.


Daktari kutoka Wizara ya TAMISEMI Dkt.Mary Shadrack akifafanua jambo.

                                   **********************************************
                                                Na.Swaum Katambo
                                                Site Tv - Katavi.

Mkoa wa Katavi umejipanga kuanzisha Huduma Mkoba ambayo itawafuata Wananchi maeneo mbalimbali ya Mikusanyiko ikiwemo sehemu za Ibada,Vituo vya mabasi,Mikutano,Magulio na maeneo mengine kwa ajili ya kutoa Elimu ya chanjo na kuwapatia huduma ya chanjo.

Akizungumza na Wanahabari Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amesema kuwa wamegundua kuna baadhi ya maeneo Wananchi wanashindwa kupata huduma ya chanjo kutokana na kukosa muda wa kwenda kwenye Kituo cha kutolea Huduma za Afya.

"Mkoa wetu ni Mkoa wa Vijijini zaidi unakuta kituo cha kutolea huduma kipo mbali,kwahiyo mwingine anakosa nauli au muda,basi tumejitolea kuwapelekea pale walipo ili kuhakikisha kwamba huduma hii sasa tunaiboresha zaidi na Mpango huu harakishi na shirikishi wa Jamii juu ya Chanjo ya UVICO-19 uweze kufanikiwa",Amesema RC Mrindoko.

Hata hivyo ameongeza kuwa mwanzoni kwa Mwezi Oktoba 2021 kutakuwa na Wiki ya chanjo,hiyo ikiwa ni mojawapo ya hamasa lakini wataendelea na makundi mbalimbali kufanya uhamasishaji ili itakapofika Wiki ya Kwanza ya Mwezi Oktoba wahakikishe kuwa wameshawafikia Wananchi wengi zaidi kwa kuwapa Elimu pamoja na hamasa ya uchanjaji.

Nae Boniface Makelemo mwakilishi kutoka Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) amewahakikishia Wanahabari na Wananchi kuwa chanjo ya UVICO-19 imeidhinishwa na WHO pamoja na Wataalamu wa Afya Tanzania wamejiridhisha chanjo hiyo ni salama na ndio maana imefika kwa wananchi kwa nia njema hivuonamewaomba wananchi kujitokeza kuchanja.

Daktari kutoka Wizara ya TAMISEMI Dkt.Mary Shadrack amesema kuwa lengo la kutembea mtaani na chanjo si kuidhalilisha chanjo hiyo bali ni kupeleka urahisi wa kuwafikia wananchi mahali popote walipo ili waweze kupata chanjo hiyo.

"Hadi jana kuna watu tuliowapata kutoka majumbani na hata leo tulivyo tawanyika kwa sababu tumesema ni shirikishi na harakish,i na ili iwe harakishi hatuwezi kukaa kusubiri watu waje vituoni kwa sababu si wote watakao amua kufika vituoni",Amesema Dkt.Mary.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt.Omari Sukari amesema zoezi la kuwafuata wananchi kwenye maeneo yao limewasaidia watu wengi kujitokeza kupata chanjo.

"Tunakwenda kukutana na Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi,Wataalamu wa Sekta ya Afya na Sekta nyingine mbalimbali ili kuhakikisha kwamba tunahamasishana na hatimaye nao kubeba jukumu la kuhamasisha jamii kuhusiana na umuhimu wa Chanjo na hatimaye jamii kuweza kuendelea kupokea  chanjo",Amesema Dkt.Sukari.

Kupitia Kampeni hiyo ya kuharakisha na kushirikisha Jamii,baadhi ya Wanahabari Mkoani Katavi wamejitokeza kwa hiari kupata chanjo ya UVICO-19 huku wakiwaomba Wananchi na wanahabari wengine wasio chanja kujitokeza kwani chanjo hiyo ni salama.

MWISHO.

Comments

Popular posts from this blog

WAJASIRIAMALI MPANDA WAILILIA SERIKALI KUCHELEWA UPATIKANAJI WA VITAMBULISHO

Na Swaumu Katambo, Katavi W afanyabiashara wadogo   katika stendi ya mabasi M izengo P inda wameiomba S erikali kuharakisha ugawaji wa vitambulisho ili kuep u kana na adha ya kulipa ushuru wa H almashauri ambao una   gharama  kubwa. W akizungumza na Site Tv  wajasiriamali M jini M panda wame i lalamikia H almashauri ya M anispaa ya M panda kuwatoza ushuru pasipo kuwa na utaratibu wowote . Mkurugenzi wa M anispaa ya M panda M ichael N zyungu amesema kuwa adha hiyo imetokana na kuchele we shwa kwa vitambulisho na amewataka wajasiriamali kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki. Vitambulisho vya ujasiriamali vilianzishwa na serikali maalumu kwa kuwasaidia wafanya   biashara wadogo kutoa huduma bila bugdha yoyote . MWISHO

Tufanye mabadiliko ya kina kwenye mfumo wa elimu -Mbunge Rose Tweve

KANISA KATOLIKI PAROKIA YA INYONGA LAFANYA MISA MAALUMU KUMUOMBEA DKT MAGUFULI, DC JAMILA ASISITIZA KUMUENZI KWA VITENDO

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda  ambaye pia ni  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mlele  Mhe  Jamila Yusu ph akisisitiza jambo wakati  akizungumza kwenye Misa Maalumu katika Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Mkuu wa Wilaya ya Mpanda  ambaye pia ni  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mlele  Mhe  Jamila Yusu ph akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Kanisa katoliki Parokia ya inyonga mara baada ya kumalizika  Misa Maalumu ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Kiongozi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga Padri  Maricelo Butoyi akiongoza Misa Maalumu ya  kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Sehemu ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga wakifuatilia ibada Maalumu ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Sehemu ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga wakifuatilia ibada Maalumu ...