Na.Swaum Katambo,
Site Tv - Katavi.
Ikiwa ni Wiki ya kusafisha fukwe ulimwenguni kote,Watumiaji wa Ziwa Tanganyika katika Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi wameombwa kuzingatia matumizi bora ya fukwe ili kuendelea kuwa na uhifadhi wa Mazingira katika fukwe hizo.
Akizungumza na chombo hiki Afisa Tarafa Kata ya Karema Mbonimpaye Ntiyonza Nkoronko amewaomba Watendaji wa Kata na Vijiji pamoja Wenyeviti wa Vitongoji kusimamia utunzaji bora wa fukwe pamoja na kuwa na Mpango Kazi wa kutembelea maeneo ya fukwe na kuhamasisha usafi wa mazingira.
"Hapa kuna watu wanaitwa BMU (Beach management unit) miongoni mwa Kazi walizonazo ni kusimamia hizi fukwe zisichafuliwe na matumizi bora ya fukwe hizi,ndio maana upande wa Karema wao ukikutwa unafua au unaoga ndani ya Ziwa ni faini,kama unataka kuoga chota maji kaogee nchi Kavu na kufua chota maji kafulie nchi kavu",Amesema Mbonimpaye.
Afisa Tarafa Kata ya Karema Mbonimpaye Ntiyonza NkoronkoAfisa uvuvi kutoka Shirika la Chakula Duniani (FAO) na Mratibu wa Mradi wa Fish4ACP Hashim Muumin amesema wameamua kuungana na wengine ulimwenguni kusafisha Mwalo uliopo Kata ya Ikola Tarafa ya Karema pamoja na mazingira ya fukwe hizo ambazo zimeelemewa sana na taka ngumu hasa plastiki zinazoingia katika maeneo ya uvuvi.
"Moja kati ya vitu ambavyo vinasabisha upungufu wa Samaki na matatizo katika maeneo yetu ya uvuvi ni hizi taka za plastiki,kwa sababu wakati mwingine zinazuia miale ya jua kuingia katika maji au vyanzo vya maji",Amesema Bw.Hashim.
Afisa uvuvi kutoka Shirika la Chakula Duniani (FAO) na Mratibu wa Mradi wa Fish4ACP Hashim Muumin.Bw.Hashim ameongeza kuwa lengo la mradi huo ni kupunguza changamoto zilizopo, kuanzia kwa mvuvi hadi kwa mlaji katika Ziwa Tanganyika pamoja na kuutambulisha Mradi katika Mkoa wa Katavi.
Comments
Post a Comment