Skip to main content

WANANCHI KATAVI WAFURAHIA CHANJO YA UVICO-19,RC AZINDUA.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi.Mwanamvua Mrindoko akiwa tayari kupata Chanjo ya UVICO-19.

Mganga Mkuu Mkoa wa Katavi Dkt.Omary Sukari akipata Chanjo ya UVICO-19.

Katibu wa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bw.Geaorge akipata Chanjo ya UVICO-19.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Benjamin Kuzaga akipata Chanjo ya UVICO-19.

                  *************************************

                    Na Mwandishi Wetu,Mpanda-Katavi.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi.Mwanamvua Mrindoko Jana Agosti 4,2021 alizindua zoezi la Uchanjaji wa Chanjo ya Jenseen (JJ) katika Mkoa huo dhidi ya UVICO-19 kwa sura mpya baada ya Watu kuitikia tofauti na ilivyodhaniwa kutokana na dhana ya kila Mtu kuhusu Chanjo hiyo.

Wakishuhudia baadhi ya Wananchi waliopata Chanjo hiyo Said Amour Arfi (Mbunge mstaafu 2005/2010-2010/215) amesema haoni haja ya Watu kutopata Chanjo kwani hakuna kitakachokukinga na Ugonjwa huo zaidi ya Chanjo.

Aidha,Arfi amewaondoa hofu wale wanaohofia kwenda kupata chanjo kwani hiyo ni kwa ajili ya Afya ya Mtu mwenyewe na Taifa kwa ujumla.

"Watu waondoe woga,wajitokeze tu kuchanja hakuna madhara yoyote kutokana na hii Chanjo. Mimi nimechanja na nawaomba wale ambao bado hawajaamua kuchanja watafakari mara Mbili,mara Tatu waamue kuchanja kama nilivyochanja Mimi"-Alisema Said Amour Arfi.

Said Amour Arfi (aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini 2005-2015 baada ya kuchanja Chanjo ya UVICO-19.

Kwa upande wake Timothy Ruwavyo amesema anajisikia vizuri kwa kuwa anaamini ameukinga Mwili wake dhidi ya Covid-19 na amewaomba Wananchi wengine wajitokeze waachane na uvumi kuwa Chanjo hizo zinamadhara.

Catherine Bukuku kutoka Shirika la PSi katika mradi wa kuwa Mjanja Mkoani Katavi amesema mwanzoni alikuwa na woga lakini baadae akaiamini chanjo kwanza kutokana na kwamba kazi yake ni yakukutana na Watu tofauti tofauti.

"Kikubwa ni kuiamini Kwanza Chanjo,najua tulikuwa na hofu na Mimi ni Mmoja kati ya waliokuwa na hofu katika Siku ya kuchanja lakini nikijiangalia niko katika kundi maalum nakutana na Watu wengi kwenye kazi,natembelea Vituo vingi vya Afya kutokana na kazi ambazo tunazifanya"-Alisema Catherene Bukuku.

Catherine Bukuku kutoka Shirika la PSi akizungumza na Chombo hiki baada ya kupata Chanjo ya UVICO-19.

Akizungumza na Chombo hiki wakati wa uzinduzi wa Chanjo hiyo katika Kituo cha Afya Ilembo Mganga Mkuu wa Katavi Dkt.Omary Sukari amesema Chanjo hiyo anapata Mtu yoyote hata kama ni Mama mjamzito au anae nyonyesha kwani hiyo ni Chanjo kama zingine.

"Chanjo hii ya UVICO,hakuna sehemu ambayo imezuia Mjamzito kuchanja lakini tunasema Sisi kitaalam tunapima kati ya faida na hasara za Chanjo,kwa hiyo pale inapotokea tupo kwenye mazingira ambayo yanachangamoto ambayo inatulazimu lazima Mjamzito achanjwe basi atachanjwa kwa sababu hakuna sehemu inayosema Mjamzito asichanjwe"-Alisema Dkt.Sukari

Kadhalika Dkt.Sukari amesema Katika Mkoa wa Katavi zimepokelewa Chanjo Elfu Tano ambazo zimesambazwa katika Vituo 16 katika Halmashauri zote za Mkoa huo,huku akisisitiza anayetaka kuchanja lazima ajitadhimini kama yupo kwenye makundi yanayolengwa ikiwemo kuandaa Vitambulisho.

Akizindua zoezi la Uchanjaji Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi.Mwanamvua Mrindoko amesisitiza upokeaji wa Chanjo ni hiari ya Mtu mwenyewe na ni bure na hayupo Mtu atalazimishwa kuchanjwa.

RC Mrindoko amewataka Watumishi Idara ya Afya kuwa waadilifu muda wote zoezi linapoendelea na kusiwepo mazingira yoyote yanayoonyesha Mwananchi anapaswa kutoa kitu chochote.

"Chanjo hizi zinatolewa bure,kwa hiyo isije ikatokea mazingira ya kumuonyesha Mwananchi kwamba anapaswa kutoa kitu flani ili aweze kupata chanjo,Chanjo hizi ni bure kwa hiyo kila Mtu ataoata bila kulipia kitu chochote"-RC Mwanamvua Mrindoko.

Baada ya zoezi hilo kuzinduliwa,Chanjo itaendelea kutolewa katika Vituo vyote 16 ambapo leo Agosti 5,2021 baadhi ya Wananchi wameendelea kujitokeza kupata Chanjo hiyo.

MWISHO.

Comments

Popular posts from this blog

WAJASIRIAMALI MPANDA WAILILIA SERIKALI KUCHELEWA UPATIKANAJI WA VITAMBULISHO

Na Swaumu Katambo, Katavi W afanyabiashara wadogo   katika stendi ya mabasi M izengo P inda wameiomba S erikali kuharakisha ugawaji wa vitambulisho ili kuep u kana na adha ya kulipa ushuru wa H almashauri ambao una   gharama  kubwa. W akizungumza na Site Tv  wajasiriamali M jini M panda wame i lalamikia H almashauri ya M anispaa ya M panda kuwatoza ushuru pasipo kuwa na utaratibu wowote . Mkurugenzi wa M anispaa ya M panda M ichael N zyungu amesema kuwa adha hiyo imetokana na kuchele we shwa kwa vitambulisho na amewataka wajasiriamali kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki. Vitambulisho vya ujasiriamali vilianzishwa na serikali maalumu kwa kuwasaidia wafanya   biashara wadogo kutoa huduma bila bugdha yoyote . MWISHO

Tufanye mabadiliko ya kina kwenye mfumo wa elimu -Mbunge Rose Tweve

KANISA KATOLIKI PAROKIA YA INYONGA LAFANYA MISA MAALUMU KUMUOMBEA DKT MAGUFULI, DC JAMILA ASISITIZA KUMUENZI KWA VITENDO

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda  ambaye pia ni  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mlele  Mhe  Jamila Yusu ph akisisitiza jambo wakati  akizungumza kwenye Misa Maalumu katika Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Mkuu wa Wilaya ya Mpanda  ambaye pia ni  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mlele  Mhe  Jamila Yusu ph akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Kanisa katoliki Parokia ya inyonga mara baada ya kumalizika  Misa Maalumu ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Kiongozi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga Padri  Maricelo Butoyi akiongoza Misa Maalumu ya  kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Sehemu ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga wakifuatilia ibada Maalumu ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Sehemu ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga wakifuatilia ibada Maalumu ...