Skip to main content

WADAU WATOA MAONI MAREKEBISHO YA KANUNI ZA SHERIA YA EPOCA.


Naibu Katibu Mkuu wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jim Yonazi akifungua Mkutano
wa wadau wa huduma za mawasiliano ili kutoa maoni kwenye rasimu ya maboresho ya kanuni 4
za Sheria ya Udhibiti wa Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta jijini Dodoma.


Mwakilishi kutoka Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Umoja wa Haki za Kupata Taarifa
(CORI) akizungumza kwenye Mkutano wa wadau wa huduma za mawasiliano ili kutoa maoni
kwenye rasimu ya maboresho ya kanuni 4 za Sheria ya Udhibiti wa Mawasiliano ya Kielektroniki
na Posta jijini Dodoma.


Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Philip
Filikunjombe akizungumza kwenye Mkutano wa wadau wa huduma za mawasiliano ili kutoa
maoni kwenye rasimu ya maboresho ya kanuni 4 za Sheria ya Udhibiti wa Mawasiliano ya
Kielektroniki na Posta jijini Dodoma.





Baadhi ya wadau wa huduma za mawasiliano wakifuatilia mkutano uliowakutanisha wadau hao
kwa ajili ya kutoa maoni kwenye rasimu ya maboresho ya kanuni 4 za Sheria ya Udhibiti wa
Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta jijini Dodoma.

                                 **************************************

                               Na Faraja Mpina na Colnelia Munyi, DODOMA

Serikali imewakutanisha wadau wa Sekta ya Mawasiliano na Habari kujadili na kutoa maoni kwenye rasimu ya marekebisho ya kanuni nne za Sheria ya Kielektroniki na Posta (EPOCA). Kanuni hizo ni kanuni za leseni, kanuni za maudhui mtandaoni, kanuni za miundombinu ya utangazaji kidijitali na kanuni za maudhui ya redio na runinga.

Akifungua kikao hicho kilichofanyika jijini Dodoma Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi amesema kuwa Serikali imeona umuhimu wa kuwaita wadau hao ili kupata maoni yao kwasababu wao ndio watekelezaji wa kanuni hizo

Dkt. Yonazi amezungumza na wadau hao na kuwaeleza kuwa matamanio ya Serikali ni kuboresha mazingira ya watoa huduma za mawasiliano na habari nchini ili wananchi waweze kunufaika na kufaidi bidhaa na huduma bora za mawasiliano.

Ameongeza kuwa hadhira hiyo imekutana kwa ajili ya kufanya maboresho ya kanuni hizo kwa kutoa maoni yao katika maeneo ambayo yamefanyiwa mapitio hivyo ushirikiano wao na mchango wao unahitajika ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Philip Filikunjombe amesema kuwa maboresho ambayo wadau wanatolea maoni yanaenda kuleta mabadiliko katika Sekta ya Mawasiliano na Habari kwa kutenganisha kati ya watoa huduma za maudhui mtandaoni kama chombo cha habari na wale wanaotoa maudhui ambayo hayahusiani na vyombo vya habari

Amesema kuwa maboresho hayo yataenda kutatua sintofahamu ya nani anatakiwa kupatiwa leseni ya kuweka maudhui mtandaoni pamoja na kushusha ada ya leseni hizo kwa mwaka ambapo maombi ya leseni kwenye rasimu ya hiyo imeshuka kutoka shilingi laki moja hadi 50,000/= na ada ya leseni kwa mwaka imeshuka kutoka shilingi milioni moja hadi shilingi laki 5 kwa mwaka.

Aidha amezungumzia kanuni zilizopo kwa sasa zinawataka watoa huduma wa redio na runinga kuomba leseni ya kutaka maudhui yaleyale kuonekana mtandaoni lakini rasimu hiyo ya maboresho ya kanuni hawatatakiwa kuomba leseni tena ili vipindi vyao kuonekana kupitia mtandao.

Dkt. Filikunjombe amezungumzia maboresho ya kanuni hizo kuwa yanaenda kupunguza ada ya leseni ya kurusha matangazo ya redio na runinga kwa asilimia 30 na kuruhusu vituo vya redio na runinga kujiunga na vituo vingine kurusha maudhui yao bila kupata kibali kutoka TCRA isipokuwa watatakiwa kupeleka mpangilio wa vipindi unaoonesha kuwa atajiunga na kituo kingine.

Amesema kuwa maboresho hayo yanaenda kuhakikisha ving’amuzi vyote vinaonesha chaneli za bure bila kujali ni king’amuzi cha kulipia au la ili kuongeza wigo wa wananchi kupata taarifa.

Maboresho mengine yaliyofanyika ni katika vipengele vya matangazo ya mubashara na kuruhusu runinga za kulipia kuchukua matangazo na kubadili leseni ya redio na runinga za jamii kutoka leseni kubwa kwenda kuwekwa kwenye kundi la leseni ndogo.

Aidha, wadau mbalimbali walitoa maoni kuhusu rasimu ya kanuni hizo kwa makundi wakiwemo wadau kutoka Umoja wa Haki ya Kupata Taarifa (CORI), Baraza la Habari Tanzania (MCT), MISA Tanzania, Umoja wa Makampuni ya Simu Tanzania (TAMNOA),Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT), Wamiliki wa Ving’amuzi na Jukwaa la Wahariri Tanzania

Kanuni nne zilizofanyiwa maboresho ni miongoni mwa kanuni 22 za mawasiliano na utangazaji zinazosimamiwa na TCRA ambapo kanuni 18 zipo chini ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na kanuni 4 zipo chini ya Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Comments

Popular posts from this blog

Mkuu wa Mkoa wa Katavi akibidhiwa Ofisi,aelezwa Miradi ya kusimamia.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi,Mwanamvua Hoza Mrindoko wa kwanza Kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera wakati wa makabidhiano ya Ofisi. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi Beda Katani. Wakuu wa Wilaya,Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Rachel Kasanda. Na Mwandishi Wetu,Site Tv Mapema leo Mei 25,2021 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko,amekabidhiwa Ofisi na aliye kuwa Mkuu wa Mkoa huo Juma Zuberi Homera aliye hamishiwa Mkoani Mbeya kuwa Mkuu wa Mkoa. Katika makabidhiano hayo,Homera amemtajia Mkuu wa Mkoa wa Katavi miradi ambayo inatakiwa kusimamiwa hadi ikamilike ni pamoja na Bandari ya Karema,Hosipitali ya Rufaa Mkoa,Kiwanda cha Nguo,Jengo la Utawala pamoja na Umeme wa Gridi ya Taifa. Aidha,amesema Katavi ni Nyumbani hivyo atatoa ushirikiano kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi huku akiwakaribisha Viongozi na Wananchi kwa ujumla katika Mkoa wa Mbeya. "Kuna hili la Gridi ya Taifa ambalo linaendelea,kuna Kiwan...

Tabasamu hili kwa Wanafunzi,Nuru imewaka Juu yao/Mwekezaji afanya Jambo ...

Ajira Mpya Wakaribishwa Mlele, Full Kula Bata/Makubwa yaja