Skip to main content

RC IBUGE ATOA MAAGIZO KWA WASAFIRISHAJI RUVUMA KUKABILIANA NA CORONA.

Baadhi ya Wadau wa Usafirishaji MjiniSongea wakiwa kwenye kikao na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kuzungumzia namna ya kukabiliana na UVIKO-19.

                       ******************************************

                               Na Mwandishi Wetu-Ruvuma.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ameviagiza vyombo vyote vya usafirishaji abiria yakiwemo malori,kuhakikisha wanaweka vipukusa mikono (sanitizers) ili kupunguza maambukizi ya UVIKO 19.

RC Ibuge ametoa maagizo hayo wakati anafunga kikao cha wadau wa usafiri na usafirishaji kilichofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea ambapo pia yamepitishwa maazimio ambayo yanahitaji utekelezaji wa pamoja.

Maazimio na maelekezo mengine ni lazima abiria wote wavae barakoa ambapo RC Ibuge amesisitiza ni lazima kila mmoja kulinda afya yake na ni wajibu wa kumlinda mwingine dhidi ya UVIKO 19.

“Ukikiuka kumlinda mwingine maana yake umevunja sheria na ni kosa la jinai ambalo halina tofauti na kukusudia kuua kwa hiyo sio hiari,unapopanda chombo cha moto uhakikishe una barakoa’’,alisisitiza Ibuge.

Mkuu wa Mkoa pia ameagiza kila stendi ya mabai ziwekwe ndoo za kutosha zenye maji tiririka na sabuni kwenye maeneo muhimu ya kuingilia na kutoka magari na yeyote ambaye anakiuka afikishwe kwenye vyombo vya sheria.

Ameagiza elimu endelevu ya kukabiliana na UVIKO 19 itolewe na wataalam wa afya kupitia redio za kijamii zilizopo mkoani Ruvuma ili wananchi wapate uelewa wa kutosha kuhusu ugonjwa huo.

Hata hivyo amesema stendi ya Mfaranyaki mjini Songea isitumike kubeba abiria kwa sababu ya kuwepo kwa kituo cha mafuta ambacho kinaweza kusababisha maafa makubwa kwa wananchi likitokea tatizo kama moto.

Akizungumzia utekelezaji wa sheria ya abiria kufunga mikanda na abiria wote kukaa kwenye viti bila kusimamishwa,Brigedia Jenerali Ibuge amesema ni muhimu kuzingatia sheria ili kupunguza msongamano kwenye vyombo vya abiria hivyo kupunguza maambukizi.

Kuhusu madereva bodaboda kubeba abiria zaidi ya mmoja,Mkuu wa Mkoa amesema suala hilo halina mjadala ni marufuku kubeba mishikaki na kwamba kofia kwa abiria ni lazima ili kujikinga.

Ametoa rai kwa wananchi wote mkoani Ruvuma kuchanja chanjo ya UVIKO 19,hata hivyo amesema chanjo hiyo ni hiari na kwamba chanjo hiyo imethibitika kitaalam inasaidia kushitua kinga ya mwili kukabiliana na UVIKO 19 hivyo kupunguza vifo au mgonjwa kuzidiwa hadi kuwekewa gasi ya kupumlia.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Agosti 6,2021

Comments

Popular posts from this blog

Mkuu wa Mkoa wa Katavi akibidhiwa Ofisi,aelezwa Miradi ya kusimamia.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi,Mwanamvua Hoza Mrindoko wa kwanza Kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera wakati wa makabidhiano ya Ofisi. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi Beda Katani. Wakuu wa Wilaya,Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Rachel Kasanda. Na Mwandishi Wetu,Site Tv Mapema leo Mei 25,2021 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko,amekabidhiwa Ofisi na aliye kuwa Mkuu wa Mkoa huo Juma Zuberi Homera aliye hamishiwa Mkoani Mbeya kuwa Mkuu wa Mkoa. Katika makabidhiano hayo,Homera amemtajia Mkuu wa Mkoa wa Katavi miradi ambayo inatakiwa kusimamiwa hadi ikamilike ni pamoja na Bandari ya Karema,Hosipitali ya Rufaa Mkoa,Kiwanda cha Nguo,Jengo la Utawala pamoja na Umeme wa Gridi ya Taifa. Aidha,amesema Katavi ni Nyumbani hivyo atatoa ushirikiano kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi huku akiwakaribisha Viongozi na Wananchi kwa ujumla katika Mkoa wa Mbeya. "Kuna hili la Gridi ya Taifa ambalo linaendelea,kuna Kiwan...

Tabasamu hili kwa Wanafunzi,Nuru imewaka Juu yao/Mwekezaji afanya Jambo ...

Ajira Mpya Wakaribishwa Mlele, Full Kula Bata/Makubwa yaja