![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjdv9FV-8cLY64F_H-J5YalGOCjdD_QVGJz_mCjPfyEMdsqYkLxS1hA6XGuFxXiI3dHBTcAlMWlIHwNTiWM-8gxF_-0HAJ8C-KfdDwCQk-mmm1xM9xlvaI_YghlPGzIGu5hN1LwynXw59E/w640-h360/vlcsnap-2021-08-23-08h17m23s154.png)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEijMIph_hDBV4nLapDyJ_xW0xaiF7C9BasmWE2lYscsBY0lbMUooq6NfjHzJ76GTHgO0IuMcLuUbWAy-qF9oyNxKqk_5t9_VReX1Y3gCuQiZOxh8mWIanl5ALw4ArHyue095Wb_M87e5j8/w640-h360/vlcsnap-2021-08-23-08h17m31s2.png)
Eneo la Karema unapojengwa Mradi wa Bandari.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgpdMmmXFu_CQQ_awrO0TBlmOi9bQaaf2PckIfhyFhYxwSITPWz8j9hxmlF5ECVu3kl7pRojE6Hq4yJGEnEmkUsDuB2quM-jnSfD6mTancpmCDe_Nhj6vE_UBY9-5D8VM2cT9RaL2DC7GE/w640-h360/vlcsnap-2021-08-23-08h17m48s171.png)
Kiwanda cha Kuchakata Pamba (NGS) kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhwG26I5Lvp_It-MPLdShRf0MJ-U1KBtNuNr4G5BIDTY6GZtHQXmzEkAydJsoO0vQpLsrAmp_YZ4Yul3plwUaAWe3EiNzqZGYJUmeeZ4GzlWtL-QHwCGogKFiDRXYkhM0zuhvKkZs-nkI8/w640-h360/vlcsnap-2021-08-23-04h05m29s56.png)
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake kuhusu ujio wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
*******************************
Na Mwandishi Wetu,Site Blog.Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa anatarajia kufanya ziara ya Siku Tatu Mkoani Katavi ambapo atatembelea,kukagua na kuzindua Miradi mbalimbali ikiwemo Bandari ya Karema sanjari na kutembelea na kuzindua Kiwanda cha Kuchakata Pamba kilichopo Halmashauri ya Wilaya Tanganyika.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake leo Agosti 23,2021 Mkuu wa Mkoa huo Bi.Mwanamvua Mrindoko amesema ziara hiyo ya Waziri Mkuu itaanza Tarehe 25-27 Agosti Mwaka huu ambapo amewaomba Wananchi kujitokeza katika maeneo yao kumlaki kwa kumshangilia Barabarani huku tahadhari za kujikinga na Virusi vya Corona zikichukuliwa.
"Naomba kuchukua nafasi hii kuwafahamisha rasmi Wananchi wote wa Mkoa wa Katavi kwamba tutapokea ugeni huu Mkubwa wa Kitaifa kwa Tarehe nilizozitaja (25-27,8,2021). Maeneo ambayo atayatembelea na kazi kubwa atakazozifanya ni za kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo na Mradi wa kwanza atakao ukagua ni Mradi wa Bandari ya Karema"-Alisema Mkuu huyo wa Katavi.
Aidha,Waziri Mkuu anatarajiwa kukagua Kituo cha Afya cha Mishamo ambapo pia atazungumza na Viongozi wa eneo la Mishamo ambalo ni Makazi ya Wakimbizi na terehe 27 Waziri Mkuu atatembelea Mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa na kisha atakagua Ujenzi wa Barabara ya kutoka Mpanda kuelekea Tabora.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgifmSsrZ3RsXcJ1ZryrCAkfpHluG_LvOQDHM9VuwTbA3vqXBBtWS60JEQZU76eSxMjdqGPUFDzxbi_r5MK_V5hnfGKe5_gCe7b4-AbkRCJA6Ie5-68JiuITabUNY2Rd1GX1KFoc2RTEv8/w640-h360/vlcsnap-2021-08-23-08h18m27s43.png)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjmFLBnc-bQl5BkXkU8G8HlIXpOC9_LLQZOiq25z1uGuOgB-2CtuMxgHMGGagHkQGSuAr2_3WcZt58grxIEkJrIHGHII1JbL9_rdob4YK89MeIBkTu8VyQtR6zntAWmmySufRsD8wfR4Lg/w640-h360/vlcsnap-2021-08-23-08h19m00s114.png)
Mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi utakaotembelewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEipT7PC-SUCZ5SyNZfSbzISnt6WaH8VB4qT8MOuDfjUF1mQEoGlOnghCYmmQBCtlGfwbAopNt6w0RL03nqA1jUBJW-zJZ308mUbnLYTnbg779eDlPH2g8WVA9WT1cF618fhPRVc5N0-TyE/w640-h360/vlcsnap-2021-08-23-08h19m28s121.png)
Barabara ya kutoka Mpanda kuelekea Tabora itakayokaguliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
"Tunawaomba Wananchi wapokee Taarifa za ujio huo na wawe katika maeneo yao kwa ajili ya kulaki ugeni huu kwa kushangilia kwa sababu hapatakuwa na Mikutano ya hadhara kutokana na hali ya uwepo wa Covid,lakini Wananchi wawe katika maeneo ya Barabara ambazo atapita ili waweze kumlaki kwa kumshangilia na kumkaribisha na wakiwa wamechukua tahadhari za kujikinga na Ugonjwa wa UVIKO"-Alisema RC Mrindoko
Katika hatua nyingine,Mhe.Mrindoko amewataka Wananchi Mkoani humo kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Ugonjwa wa Corona,na ametoa wito kwa wale ambao bado hawajachanja kufika katika Vituo vya Afya waweze kupatiwa Chamjo.
Kadhalika,amewaondoa wasiwasi Wananchi kuhusu Usalama wa Mkoa kwani hadi sasa hakuna matukio makubwa yanayotishia usalama.
MWISHO.
Comments
Post a Comment