![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjPVjj7rSZnZl8WXFd9RFSt7GPFueXb5KyST0R7p-SWY2taofd3NCJdt_LuXGBJQ6toDPRGKMdCuHtxDaVO3gy5MBKdseARKpZls4BBYVoCOmA4-04rl3fiMo20gXXq6n3Prr1CggwrCPs/w640-h360/vlcsnap-2021-08-05-03h47m04s985.png)
Bibi Godlia Maenge,Mtoa kero.
Mkuu wa Mkoa wa Ktavi,Mhe.Mwanamvua Mrindoko akitoa maelekezo.
Na Mwandishi Wetu,Mpanda-Katavi.
Licha ya Serikali kuweka mifumo mizuri ya upimaji Ardhi,bado migogoro ya Ardhi ni tatizo katika Jamii hivyo ipo haja kwa Viongozi na Wataalam kutoka maofisini kukutana na Wananchi ikibidi kutenga Siku za kusikiliza kero mara kwa mara na kuzitatua kabla Mwananchi hajafanya uwekezaji na kumsababishia hasara.
Hilo linadhihirika katika Kikao cha Kwanza cha Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi.Mwanamvua Mrindoko cha kusikiliza kero,kilichofanyika Agosti 4,2021 Ofisini kwake ambapo Asilimia kubwa ya waliowasilisha kero zao ilikuwa ni masuala ya Ardhi.
Akiwasilisha kero yake kwa Mkuu wa Mkoa,Bibi Godlia Constantino Maenge Mkazi wa Kichangani Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi amewalalamikia Mabwana Ardhi kuchukua eneo lake analoishi na kumpa Mtu mwingine huku wakimataka ahame eneo hilo kwa kile alichoelezwa ni eneo la wazi.
"Mabwana Ardhi kwenye eneo langu ninapoishi Kichangani,walilichukua wakampa Mtu mwingine Kiwanja nyuma yangu,baada ya hapo ndiyo nikaanza kulalamika juu ya huyo Baba waliempa Kiwanja tukikuja kusimama kwa Mkuu wa Mkoa wakamwambia hatuwezi tukamtoa Mkolechi (Mzee) pale tulipomkuta"-Bi.Maenge
Kutokana na kilio hicho,Mkuu wa Mkoa ametoa Siku Saba kwa Idara ya Ardhi Manispaa ya Mpanda kumtafuta huyo aliyepimiwa karibu na Bibi huyo ili ikiwezekana atafutiwe eneo lingine na alipwe fidia ampishe Bibi aendelee kuishi kwenye eneo ambalo amedai hawezi kulihama kwani ameshaliozea.
Hata hivyo,RC Mrindoko amesema anaweka utaratibu wa kila Mwezi kusikiliza Kero za Wananchi.
MWISHO.
Comments
Post a Comment