Skip to main content

BAKITA SHIRIKISHENI WADAU KUBORESHA MKAKATI WA KUBIDHAISHA KISWAHILI-WAZIRI BASHUNGWA.



PICHANI Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa katika kikao na Watendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA).

                                    *************************************************

                                        Na Projestus Binamungu-MAELEZO

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa ameliagiza Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) kuwashirikisha wadau wa lugha ya Kiswahili katika kuboresha Mkakati wa Taifa wa Miaka 10 wa Kubidhaisha Kiswahili ili uzinduluwe na kuanza kutekelezwa.

Waziri Bashungwa ametoa agizo hilo leo katika kikao na Watendaji wa Baraza hilo kilichofanyika Ofisi za BAKITA Jijini Dar es Salam ambapo aliambatana na Naibu wake Mhe.  Pauline Gekul.

Pamoja na kuagiza ushirikishwa wa wadau katika kuboresha Mkakati huo, Waziri Bashungwa pia ameiagiza BAKITA kufanya maboresho kadhaa, ikiwa ni pamoja na kuongeza ufunguzi wa vituo maalum vya kufundishia lugha ya Kiswahili na Utamaduni wa Mtanzania katika nchi mbalimbali duniani.

Mkakati huo unaopendekezwa na BAKITA unalenga kubidhaisha lugha ya Kiswahili ndani na nje ya nchi katika kipindi cha mwaka 2021-2031, ambapo lugha hiyo kwa miaka ya hivi karibuni imeanza kutumika kama lugha rasmi katika nchi mbalimbali duniani na Jumuiya za Kimataifa kama Umoja wa Afrika (AU), Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC) na Jumuiaya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).

Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Bi. Consolata Mushi, baada ya kupokea maelekezo viongozi hao, hatua inayofuata ni kuwapitisha wadau wa Kiswahili katika Mkakati huo kabla ya kuuwasilisha kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi, kwa ajili ya hatua zaidi za kiutendaji na utekelezaji wa mkakati huo.

MWISHO.

Comments

Popular posts from this blog

WAJASIRIAMALI MPANDA WAILILIA SERIKALI KUCHELEWA UPATIKANAJI WA VITAMBULISHO

Na Swaumu Katambo, Katavi W afanyabiashara wadogo   katika stendi ya mabasi M izengo P inda wameiomba S erikali kuharakisha ugawaji wa vitambulisho ili kuep u kana na adha ya kulipa ushuru wa H almashauri ambao una   gharama  kubwa. W akizungumza na Site Tv  wajasiriamali M jini M panda wame i lalamikia H almashauri ya M anispaa ya M panda kuwatoza ushuru pasipo kuwa na utaratibu wowote . Mkurugenzi wa M anispaa ya M panda M ichael N zyungu amesema kuwa adha hiyo imetokana na kuchele we shwa kwa vitambulisho na amewataka wajasiriamali kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki. Vitambulisho vya ujasiriamali vilianzishwa na serikali maalumu kwa kuwasaidia wafanya   biashara wadogo kutoa huduma bila bugdha yoyote . MWISHO

Tufanye mabadiliko ya kina kwenye mfumo wa elimu -Mbunge Rose Tweve

KANISA KATOLIKI PAROKIA YA INYONGA LAFANYA MISA MAALUMU KUMUOMBEA DKT MAGUFULI, DC JAMILA ASISITIZA KUMUENZI KWA VITENDO

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda  ambaye pia ni  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mlele  Mhe  Jamila Yusu ph akisisitiza jambo wakati  akizungumza kwenye Misa Maalumu katika Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Mkuu wa Wilaya ya Mpanda  ambaye pia ni  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mlele  Mhe  Jamila Yusu ph akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Kanisa katoliki Parokia ya inyonga mara baada ya kumalizika  Misa Maalumu ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Kiongozi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga Padri  Maricelo Butoyi akiongoza Misa Maalumu ya  kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Sehemu ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga wakifuatilia ibada Maalumu ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Sehemu ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga wakifuatilia ibada Maalumu ...