Skip to main content

MPANGO WA UBORESHAJI KILIMO CHA UMWAGILIAJI, KATAVI BADO CHANGAMOTO.




Mkulima Mdogo,Emmanuel Ramadhan.

Ramadhan Nyembe Mkulima Kijiji cha Majalila.

Baadhi ya Wakulima wakivuna Mpunga.





Magunia ya Mpunga.



PICHA  NA ZAINAB MTIMA,Site Tv

Na.Swaum Katambo,Tanganyika-Katavi.

Licha ya Serikali kuwekeza zaidi ya Bilioni 5 kwa ajili ya Skimu tatu za Umwagiliaji zilizopo Wilayani Mpanda ambazo ni Ugala,Mwamkulu na Uruila,Mkoa wa Katavi hauna Skimu iliyokamilika pamoja na kuwa Mpango wa Serikali wa Mwaka 2021/22 ni kuboresha Kilimo cha Umwagiliaji Nchini.

Hayo yanakuja mara baada ya Wakulima katika Kijiji cha Majalila Kata ya Tongwe Wilayani Tanganyika Mkoani Katavi kusikiliza Hotuba aliyoitoa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Mwigulu Nchemba kuhusu Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2021/22 katika Sekta ya Kilimo kuwa Maeneo yatakayopewa msukumo ni pamoja na ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya umwagiliaji.

"Kwa bajeti iliyosomwa inaonekana wakulima inatuinua,Serikali imetuangalia kwa macho mawili labda tusubiri utekelezaji kwa sababu yanayosemwa ni mazuri lakini kwenye utekelezaji sasa inaweza isifanye vizuri",Alisema Ramadhan Nyembe Mkulima Kijiji cha Majalila.

Nyembe ametolea mfano kwa Mkoa mzima wa Katavi kuwa una Skimu za Umwagiliaji tatu huku skimu hizo zikiwa hazijakamilika hivyo anaamini kuwa Serikali ikitilia mkazo katika Kilimo cha umwagiliaji na kuzikamilisha Skimu hizo wakulima watalima Kilimo chenye tija.

Kwa Mkoa wa Katavi Serikali ilitenga kiasi cha shilingi Bilioni 5.6 kwa Skimu tatu za Umwagiliaji ambapo Skimu ya  Ugalla ilitengewa Sh Bilioni 1.2, Skimu ya Umwagiliaji ya Mwamkulu ilitengewa Sh Bilioni 1.6 na Skimu ya Uruila ilitengewa sh Bilioni 1.8 lakini bado hazijakamilika.

Hata hivyo wakulima pia wameipongeza hatua ya Serikali kutaka kuimarisha mifumo ya upatikanaji wa pembejeo za kilimo ikiwemo zana za kilimo, mbegu bora za mazao, mbolea na viuatilifu. 

"Zamani tulikuwa tunanunuliana tuu una debe la Malamata (Mbegu ya kienyeji ya Mpunga) uniletee hapa,basi tunapanda tuu kienyeji..,lakini upatikanaji wa mbegu bora za mazao itakuwa na kipato kingi cha kutosha tofauti na tulivyozoea mwanzoni",Alisema Emmanuel Ramadhan Mkulima mdogo.

Aidha, wakulima katika Kijiji cha Majalila wameiomba Serikali kuwasogezea nyenzo au kuwapatia vifaa kwa ajili ya kuvunia mazao kwani wanapata Changamoto nyingi pindi unapofika msimu wa mavuno.

"Kama unavyoona hivi tunahangaika sana,lakini tungekuwa tunatumia mashine tungekuwa tumeshamaliza muda mrefu,tunaomba sana Serikali ituangalie hata kwa kutupa Mikopo ya Vitendea kazi tungeshukuru sana",Alisema  Nyembe.

Kwa Mujibu wa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Mwigulu Nchemba wakati akiwasilisha Bungeni Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2020 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2021/22 amesema Serikali ina Mpango wa kuongeza matumizi ya teknolojia na mbinu za kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabianchi,
kuongeza matumizi ya teknolojia bora katika uzalishaji wa mazao ili kuongeza uzalishaji na tija, kuimarisha vituo vya utafiti wa mbegu bora,vyuo vya mafunzo na vituo vya mafunzo ya wakulima na huduma za ugani. 

Kadhalika, Serikali inatarajia kuongeza thamani ya mazao ya kilimo na kuhakikisha upatikanaji wa masoko ya ndani na nje ya nchi,Vilevile itaendelea kuhamasisha uzalishaji wa mazao yakiwemo mazao ya kimkakati ya Mkonge, Chikichi, Tumbaku,Pareto,Korosho, Kahawa na Pamba. 

MWISHO.

Comments

Popular posts from this blog

Mkuu wa Mkoa wa Katavi akibidhiwa Ofisi,aelezwa Miradi ya kusimamia.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi,Mwanamvua Hoza Mrindoko wa kwanza Kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera wakati wa makabidhiano ya Ofisi. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi Beda Katani. Wakuu wa Wilaya,Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Rachel Kasanda. Na Mwandishi Wetu,Site Tv Mapema leo Mei 25,2021 Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko,amekabidhiwa Ofisi na aliye kuwa Mkuu wa Mkoa huo Juma Zuberi Homera aliye hamishiwa Mkoani Mbeya kuwa Mkuu wa Mkoa. Katika makabidhiano hayo,Homera amemtajia Mkuu wa Mkoa wa Katavi miradi ambayo inatakiwa kusimamiwa hadi ikamilike ni pamoja na Bandari ya Karema,Hosipitali ya Rufaa Mkoa,Kiwanda cha Nguo,Jengo la Utawala pamoja na Umeme wa Gridi ya Taifa. Aidha,amesema Katavi ni Nyumbani hivyo atatoa ushirikiano kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi huku akiwakaribisha Viongozi na Wananchi kwa ujumla katika Mkoa wa Mbeya. "Kuna hili la Gridi ya Taifa ambalo linaendelea,kuna Kiwan...

Tabasamu hili kwa Wanafunzi,Nuru imewaka Juu yao/Mwekezaji afanya Jambo ...

Ajira Mpya Wakaribishwa Mlele, Full Kula Bata/Makubwa yaja