Na Swaum Katambo-Katavi
Mkoa wa Katavi leo Aprili 14, 2020 umetimiza agizo la aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa ziarani Mkoani Katavi mnamo Octoba 10, 2019 ambapo aliagiza uanzishwaji wa mabucha ya nyamapori nchini.
Akizindua Bucha hilo la nyamapori Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Homera ametumia fursa hiyo kuwaasa wananchi kutojihusisha na matukio ya ujangili kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria huku akitaja bei elekezi ya nyama hizo kuwa ni shilingi 8000 kwa kilo moja.
Kwa upande wake meneja wa Pori la Akiba (TAWA) Mkoa wa Rukwa Baraka Balagaye amesema wako tayari kushirikiana na wananchi watakaohitaji kufunga mabucha ya nyamapori ikiwa ni pamoja na kutoa miongozo isiyo na masharti magumu.
Hata hivyo Mmiliki wa Bucha lililozinduliwa Ndugu Vedasto Magaba ameishukuru Serikali na Taasisi mbalimbali kwa ajili ya kufanikisha adhma ya kufungua Bucha la nyamapori ikiwa ni Bucha la kwanza kwa Mkoa wa Katavi tangu tamko la Hayati Dkt Magufuli alipoelekeza kuanzishwa kwa mabucha hayo nchini huku akielezea changamoto ya upatikanaji wa wanyamapori kutokana na kipindi cha mvua za Masika wanyama kuwa mbali zaidi na kutopatikana kwa urahisi hali inayopelekea kutumia gharama kubwa.
Kwa upande wao wananchi wamemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe Homera kwa kusimamia uanzishwaji wa Bucha la nyamapori huku wakiomba huduma hiyo kuwa endelevu kadhalika na wahusika kupunguza bei kutoka ya shilingi 8000 hadi shilingi 7000 kwa siku za mbeleni ili kukidhi mahitaji ya wananchi wa hali ya chini.
MWISHO
Comments
Post a Comment