Abiria Mkoani Katavi wameishukuru Kampuni ya Mabasi Adventure Connection kwa kurudisha safari za mabasi kutoka Katavi kwenda Dar es Salaam ambapo zilisitishwa kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo hivyo kupelekea kupata changamoto ya usafiri.
Wakizungumza na Site Tv abiria hao wamesema hapo awali kulikuwa na changamoto hasa kwa abiria wanaohitaji kwenda mikoa ya Dodoma, Morogoro,Pwani na Dar es Salaam kutokana na kutokuwepo kwa usafiri wa moja kwa moja hivyo kupelekea kulala Tabora jambo ambalo lilikuwa likiwagharimu muda na fedha nyingi zikiwemo za chakula na malazi.
Kwa upande wake Msimamizi wa Kampuni ya Mabasi ya Adventure Connection Tawi la Mpanda Nassor Ally amesema walisitisha safari hizo kwa kipindi cha miaka miwili kutokana na changamoto za uendeshaji pamoja na Miundombinu ya barabara kutokuwa rafiki lakini kwa sasa wamejidhatiti ili kuhakikisha changamoto walizokabiliana nazo hazijitokezi tena.
Kadhalika, amewaasa abiria kutodanganyika na wapiga debe wa stendi ambao huwadanganya hakuna usafiri wa moja kwa moja kwenda Dar kwa lengo la kuwatapeli.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Stendi ya Mizengo Pinda Katavi Edward Gelard amewashauri wawekezaji waongeze mabasi ya abiria mkoani hapa kwa kuwa abiria ni wengi na mabasi ni machache.
MWISHO
Comments
Post a Comment