Na, Swaum Katambo-Katavi Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Homera ametoa siku 7 kwa wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Tanganyika,Nsimbo na Mlele kuwasilisha fedha za ujenzi wa Eneo la maonesho ya wakulima Nanenane lililopo Kata ya Kabungu Wilayani Tanganyika. Maagizo hayo yametolewa leo Aprili 19,2021 katika kikao cha wadau wa Sekta ya Kilimo Mkoa wa Katavi kilichofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Maji uliopo Manispaa ya Mpanda mara baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Afisa Kilimo wa Mkoa Faridu Mtiru alipokuwa akiwasilisha maadhimio yatokanayo katika kikao cha wadau wa Kilimo kilichoketi mnamo Desemba 16,2020. Hata hivyo RC Homera amewaambia Wakuu wa Wilaya pamoja na Wakurugenzi endapo watashindwa kutekeleza agizo hilo waandike maelezo ya kushindwa kutekeleza huku akiwapongeza Manispaa ya Mpanda pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe ambao wamekwisha wasilisha fedha zao. Kadhalika katika kikao hicho kilichokutani...