Na; Mwandishi Wetu– Kagera
Ukarabati wa Miundombinu ya Kilimo cha umwagiliaji Wilayani Karagwe Mkoani Kagera Umeanza Rasmi, kwa ujenzi wa Barabara katika skimu ya kilimo cha umwagiliaji Mwisa pamoja na mifereji ya kupitisha maji kuelekea mashambani.
Akizungumza wakati wa kupokea vifaa vya ujenzi Mhandisi wa Umwagiliaji, ambaye pia ni Meneja Maradi huo shirikikishi Bw. Adelialidy Mwesigwe, Amesema amepokea baadhi ya viaafa ambavyo vitaweza kutumika katika ujenzi pamoja na kusakafia mfereji wenye urefu wa mita mia saba hamsini (750), ambapo mpaka sasa mtaro wenye urefu wa mita mia tano na mbili (502) umeshachimbwa na barabara yenye urefu wa mita mia saba na sitini (760) inayokwenda sambamba na mtaro huo imekwisha andaliwa.
“Tutajenga vikinga maji tisa, (9) kwenye awamu hii kutokana na kwamba skimu hii ina ukubwa wa eneo la Hekta mia tatu (300) ambalo linalimwa zao la mpunga na mazao mchanganyiko.” Alisema Mwesigwa.
Aliendelea kusema kuwa eneo ambalo lpo nje kidogo wakulima wanalima bustani za mbogamboga, na Skimu ina idadi ya wakulima mia moja na sabini na tano (175).
Miradi hii shirikishi ya maendeleo ya serikali ya awamu ya tano katika sekta ya kilimo cha umwagiliaji inashirikisha wananchi wakazi wa eneo husika katika ujenzi na ukarabati wa miundombinu hiyo.
MWISHO
Comments
Post a Comment