Skip to main content

TUME YA MADINI YAFIKISHA ASILIMIA 75.8 UKUSANYAJI WA MADUHULI KWA MWAKA 2020-2021





Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba amesema kuwa kuanzia kipindi cha mwezi Julai, 2020 hadi Februari 2021 katika mwaka wa fedha 2020-2021, Tume ya Madini ilifanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 399.3 ikiwa ni sawa na asilimia 75.8 ya lengo la kukusanya shilingi bilioni 526.7.

Mhandisi Samamba ameyasema hayo leo tarehe 04 Machi, 2021 kwenye kikao chake na Kurugenzi ya Ukaguzi wa Migodi na Mazingira iliyopo chini ya Tume ya Madini jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya ziara yake kwenye Kurugenzi na Vitengo kwa ajili ya kusikiliza na kutatua changamoto za utendaji kazi pamoja na kuweka mikakati ya ukusanyaji wa maduhuli na uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji kwenye Sekta ya Madini.

Amesema kuwa Tume ya Madini bado inaendelea kuweka mikakati ya kuzuia mianya yote ya utoroshaji wa madini, ukusanyaji wa maduhuli, uboreshaji wa masoko ya madini sambamba na usimamizi wa afya na mazingira kwenye migodi ya madini.

Katika hatua nyingine, Mhandisi Samamba amewapongeza watumishi wa Kurugenzi ya Ukaguzi wa Migodi na Mazingira kwa kazi nzuri ya usimamizi na ukaguzi wa mazingira na afya kwenye migodi ya madini hali iliyopelekea kupungua kwa ajali na athari za mazingira kwenye shughuli za uchimbaji wa madini.

"Zamani kulikuwa na ajali za mara kwa mara kwenye migodi ya madini lakini kwa sasa ajali zimekuwa ni chache sana, hongereni sana na muendelee kuweka mikakati zaidi kwani nia yetu kama Serikali ni kuhakikisha watanzania wananufaika na rasilimali za madini pasipo kupata athari za aina yoyote," amesema Mhandisi Samamba.

Katika ziara yake, Mhandisi Samamba ameshatembelea Kurugenzi ya Leseni na TEHAMA na Kurugenzi ya Ukaguzi na Biashara ya Madini.

Comments

Popular posts from this blog

WAJASIRIAMALI MPANDA WAILILIA SERIKALI KUCHELEWA UPATIKANAJI WA VITAMBULISHO

Na Swaumu Katambo, Katavi W afanyabiashara wadogo   katika stendi ya mabasi M izengo P inda wameiomba S erikali kuharakisha ugawaji wa vitambulisho ili kuep u kana na adha ya kulipa ushuru wa H almashauri ambao una   gharama  kubwa. W akizungumza na Site Tv  wajasiriamali M jini M panda wame i lalamikia H almashauri ya M anispaa ya M panda kuwatoza ushuru pasipo kuwa na utaratibu wowote . Mkurugenzi wa M anispaa ya M panda M ichael N zyungu amesema kuwa adha hiyo imetokana na kuchele we shwa kwa vitambulisho na amewataka wajasiriamali kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki. Vitambulisho vya ujasiriamali vilianzishwa na serikali maalumu kwa kuwasaidia wafanya   biashara wadogo kutoa huduma bila bugdha yoyote . MWISHO

Tufanye mabadiliko ya kina kwenye mfumo wa elimu -Mbunge Rose Tweve

KANISA KATOLIKI PAROKIA YA INYONGA LAFANYA MISA MAALUMU KUMUOMBEA DKT MAGUFULI, DC JAMILA ASISITIZA KUMUENZI KWA VITENDO

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda  ambaye pia ni  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mlele  Mhe  Jamila Yusu ph akisisitiza jambo wakati  akizungumza kwenye Misa Maalumu katika Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Mkuu wa Wilaya ya Mpanda  ambaye pia ni  Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mlele  Mhe  Jamila Yusu ph akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Kanisa katoliki Parokia ya inyonga mara baada ya kumalizika  Misa Maalumu ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Kiongozi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga Padri  Maricelo Butoyi akiongoza Misa Maalumu ya  kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Sehemu ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga wakifuatilia ibada Maalumu ya Kumuombea Hayati Dkt John Pombe Magufuli, tarehe 24 Machi 2021. Sehemu ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Inyonga wakifuatilia ibada Maalumu ...